loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga dhaifu, Simba imara

WAKATI vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakionesha udhaifu katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar kwa kufungwa 1-0, watani zao Simba wameendelea kula `viporo’ vyao vizuri baada ya jana kushinda 2-1 dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Yanga wameendelea kupoteza pointi baada ya jana kukubali kichapo hicho katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa na kulipa kisasi cha kufungwa 2-1 katika mchezo uliopigwa Agosti mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Bao hilo pekee katika mchezo huo liliwekwa kimiani katika dakika ya 52 lililofungwa na Riphat Msuya akitumia udhaifu wa safu ya ulinzi ya timu ya Yanga na kupinga shuti kali lililomshinda kipa Klaus Kindoki na kujaa wavuni.

Kutoka na ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 48 baada ya kucheza mechi 32 na kupanda hadi nafasi ya nne kutoka ya tano, na kuishusha chini timu ya Lipuli FC ya Iringa. Pamoja na kichapo hicho, Yanga inaendelea kuongoza katika msimamo wa ligi hiyo kwa kuwa na pointi 74 baada ya kucheza mechi 32, ikiwa imepoteza mechi nne hadi sasa msimu huu na kuzidi kutoa nafasi kwa Simba kuwa katika nafasi nzuri ya kutetea taji lake.

Licha ya kufungwa na Mtibwa Sugar katika mchezo huo Yanga iliweza kuandika bao dakika ya 85 lililofungwa kupitia kwa Amiss Tambwe akimalizia pasi ya kichwa cha Mrisho Ngassa lakini mwamuzi alikataa akidai kuwa mfungaji aliotea. Katika kipindi cha kwanza, dakika ya pili mchezaji wa Yanga, Heritier Makambo aliokoa kuifungia timu yake bao baada ya shuti lake kuokolewa na kipa wa Mtibwa Sugar, Shaaban Kado.

Kwa upande wa Simba, wenyewe waliendelea kuunguruma baada ya kuichapa 2-1 Coastal Union katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga na kufikisha pointi 60 baada ya kucheza mechi 23.

Wenyeji Coastal Union ndio walikuwa wa kwanza kufunga kupitia kwa chipukizi wake, Raizin Hafhid aliyetumia makosa ya Erasto Nyoni aliyechanganyana na kipa wake, Aishi Manula kabla ya Simba kusawazisha na kufunga la ushindi kupitia kwa Meddie Kagere. Hiyo ni mechi ya kwanza ya Ligi Kuu kwa Simba tangu ilipotolewa na TP Mazembe kwa jumla ya mabao 4-1 katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika.

WASANII sasa mambo yao safi baada ya serikali kuwarahisishia utendaji ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi