loader
Picha

Masikini Serengeti Boys

TIMU ya taifa ya Tanzania, Serengeti Boys jana ilijiweka katika nafasi fi nyu katika mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Uganda kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Uganda waliandika bao lao la kwanza katika dakika ya 15 lililofungwa na Kawooya Andrew akiunganisha wavuni krosi ya Najibu Viga huku lile la pili likifungwa na Asaba Ivan katika dakika ya 27 Najib Yiga.

Serengeti Boys iliendelea kulala, Yiga aliifungia Uganda bao la tatu na la ushindi na kuifanya Serengeti kushika mkia katika Kundi A na kuacha simanzi kwa wapenzi wa soka nchini. Serengeti Boys inasubiri mchezo wa mwisho dhidi ya Senegal huku Nigeria ikisonga mbele baada ya kushinda mchezo wake wa awali kwenye uwanja huo na kufikisha pointi sita baada ya kushinda ule wa ufunguzi dhidi ya Tanzania.

KABLA ya Yanga kukutana na As Vita ya DR. Congo ...

foto
Mwandishi: Mohammed Akida

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi