loader
Picha

Serikali yaeleza sababu hospitali ya Mirembe kujengwa Dodoma

HOSPITALI ya Rufaa la Kitaifa ya Mirembe haikujengwa mkoani Dodoma kutokana na mkoa huo kuwa na wagonjwa wengi wa akili (vichaa) bali kutokana na kuwepo kwa Gereza la Isanga ambalo wanafungwa wahalifu wakubwa na wauaji na hutakiwa kupima akili zao, serikali yaeleza leo Bungeni, Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendelelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile alitoa kauli hiyo kutokana na Spika Job Ndugai kutaka kujua kama habari za kwamba hospitali hiyo ya kutibu wagonjwa wa akili ilijengwa mkoani hapo kutokana na Dodoma kuwa na wagonjwa wengi wa akili.

Dk Ndugulile alisema hospitali hiyo ilijengwa mkoani hapo hapo kutokana na mkoa huo kuwa na gereza kubwa la Isanga ambalo lina wafunga wa wauaji na wahalifu wakubwa ambao hutakiwa kupimwa pia akili zao.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) aliyetaka kujua kwanini kuna uhaba wa dawa za kutibu kifafa na magonjwa ya akili wilayani Ulanga wakati wilaya hiyo inaongoza nchini kwa kuwa na wagonjwa wengi wa maradhi hayo.

Dk Ndugulile alisema ni kweli katika mkoa wa Morogoro hasa wilaya ya Ulanga kuna wagonjwa wengi wa kifafa na akili lakini atafuatilia ili kujua kwanini dawa hizo zinakwama kufika huko wakati zipo za kutosha. Taarifa zaidi itachapishwa kwenye gazeti la HabariLeo kesho, Ijumaa

MTAALAMU wa masuala ya afya na lishe kutoka shirika lisilo ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi