loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Saba kortini kwa kutumia vibaya jina la mke wa Rais

WAKAZI saba wa Jiji la Dar es Salaam, wamefi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka mbalimbali, ikiwemo kuchapisha taarifa za uongo katika mtandao wa kijamii wa Facebook kwa kutumia jina la mke wa Rais, John Magufuli, Mama Janeth.

Washitakiwa hao ni Saada Uledi, Maftaha Shaban, Heshima Ally, Shamba Baila, Fadhili Mahenge, Obadia Kwitega na Stella Omary, ambao walisomewa mashitaka kwa mahakimu wanne tofauti. Washitakiwa hao walisomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, Wanjah Hamza, Augustine Rwizile na Janeth Mtega.

Akisoma mashitaka, Wakili wa Serikali, Batilda Mushi alidai mbele ya Hakimu Kasonde kuwa, kati ya Januari 2017 na Machi mwaka huu, jijini Dar es Salaam na maeneo mengine ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, washitakiwa Saada, Shaban, Ally na Baila walikula njama ya kuchapisha maneno au taarifa za uongo kupitia ukurasa wao wa Facebook.

Katika mashitaka ya pili, Mushi alidai kuwa washitakiwa hao walichapisha machapisho katika ukurasa huo wa Facebook kuwa Mama Janeth ameunda taasisi inayofanya kazi ya kukopesha na kutoa mkopo kwa watu, ikiwa na masharti yanayowataka watu hao kuweka fedha kama dhamana ya kupata mkopo huo.

Alidai mashitaka ya tatu kuwa kati ya Machi 2 na Machi 8, mwaka huu jijini Dar es Salaam, washitakiwa hao wakiwa kama waendeshaji wa ukurasa huo, uliosajiliwa kwa jina la Janeth Magufuli, kwa nia ya kudanganya na kupotosha na kwa kutumia uhamisho wa fedha kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine walijipatia Sh 4,487,000.

Washitakiwa hao walijipatia fedha hizo kutoka kwa Simon Kunambi, kama ulinzi au dhamana ya mkopo, ambao angepatiwa kutoka kwenye taasisi hiyo ya mke wa Rais, huku wakijua kuwa si kweli. Katika mashitaka ya nne, siku na mahali hapo, washitakiwa hao walijipatia kiasi hicho cha fedha huku wakijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mbele ya Hakimu Hamza, inadaiwa kati ya Januari 2017 na Machi mwaka huu mshitakiwa Mahenge akiwa Dar es Salaam, Rukwa, Songwe na sehemu nyingine za Tanzania, alisambaza taarifa za uongo kwa kutumia ujumbe wa tuma pesa kwenye namba hii huku akijua ujumbe huo ni wa uongo uliokuwa na nia ya kupotosha umma. Mshitakiwa huyo pia anadaiwa katika siku na mahali hapo, alianzisha na kusambaza ujumbe bila ridhaa ya mpokeaji kwa kutumia laini za simu ambazo amezisajili kwa jina lake kupitia mitandao tofauti tofauti.

Pia, anadaiwa akiwa ndani ya Tanzania na nje ya nchi alisambaza ujumbe kwa watu mbalimbali kwa nia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Mahenge anadaiwa kwa njia ya udanganyifu kwa kutumia simu ya mkononi, kupitia laini zipatazo 629 ambazo zilikuwa zimesajiliwa kwa jina lake alijipatia Sh milioni 123 kutoka kwa watu mbalimbali huku akijua analolifanya si la kweli. Mshitakiwa huyo anadaiwa kutakatisha fedha kwa kujipatia Sh milioni 123, huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udang-

IKIWA fomu moja ya kuomba ridhaa ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi