loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TMA yatoa utabiri mpya mvua, joto

MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imesema katika kipindi cha wiki mbili za mwisho wa Aprili, mwaka huu, hali ya joto inatarajiwa kuwa ya kawaida katika maeneo ya Pwani ya Kaskazini na Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki hususani katika kipindi cha uwepo wa mvua.

Imesema maeneo mengi ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara yanatarajiwa kuendelea kuwa na upungufu wa vipindi vya mvua. Kwa mujibu wa taarifa ya TMA, kwa wadau wa hali ya hewa nchini, vipindi vichache vya mvua vinatarajiwa kuendelea katika maeneo ya Ukanda wa Pwani kwa wiki ya tatu na ya nne ya Aprili.

Ilieleza kuwa maeneo ya Ukanda wa Ziwa Victoria, vipindi vya mvua za kawaida vinatarajiwa kuendelea kwa kipindi chote cha mwezi kilichosalia. Taarifa hiyo iliongeza kuwa kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa na Morogoro Mahenge, Kigoma Katavi, Tabora, Lindi na Mtwara, vipindi vya mvua za kiasi vinatarajiwa kuendelea.

Iliongeza kuwa hata hivyo ongezeko la mvua linatarajiwa katika maeneo ya mikoa ya Lindi na Mtwara hususani wiki ya mwisho mwa Aprili, maeneo ya mikoa ya Dodoma na Singida msimu wa mvua umeisha hivyo maeneo hayo yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla.

Aidha, TMA inawashauri wananchi kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka hiyo, na kuzingatia tahadhari zilizotolewa na mirejeo yake pamoja na kupata na kuzingatia ushauri na miongozo ya wataalamu katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

IKIWA fomu moja ya kuomba ridhaa ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi