loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Malecela: Watendaji serikalini msibweteke

KAULI ya Rais John Magufuli ya kuwataka watendaji wa Wizara na Idara mbalimbali za serikali kuwajibika ipasavyo katika kuhakikisha dhana ya viwanda na uwekezaji inafanikiwa, imeungwa mkono na baadhi ya viongozi wastaafu akiwemo Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela.

Malecela alisema ni kweli watendaji serikalini na katika idara nyingine za serikali hawapaswi kubweteka na badala yake wafanye kazi kwa bidii. Alisema mawaziri ambao wengi wao ni wabunge wa kuchaguliwa na wakati mwingine wanalazimika kuyatumikia majimbo yao, hivyo watendaji hawana budi kujituma. Alisema kwa kiasi kikubwa serikali iliyopo madarakani inajitahidi kufanya kazi vizuri katika kuwatumikia wananchi katika mambo ya maendeleo.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi Bara (CCM), Pius Msekwa, alisema Rais Magufuli alifanya vyema kuwakumbusha mawaziri kuhusu wajibu wao kwa taifa, lakini ana imani kuwa Ilani ya CCM itatekelezwa kwa ukamilifu. Msekwa alisema utekelezaji wa ilani ya CCM hauwezi kuathirika kwa kuwa serikali ni mfumo wenye wataalamu mbalimbali.

Alisema utendaji serikalini unaendelea wakati wote hata kipindi cha kampeni na uchaguzi, na ndiyo maana Rais Magufuli amewataka watendaji hao kuwajibika. Juzi, Rais Magufuli alitoa wiki moja kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Viwanda na Biashara kukamilisha taratibu za uwekezaji kwa Kampuni ya Sugar Investment Trust (SIT) ya Mauritius ambayo imecheleweshwa kuwekeza katika uzalishaji wa sukari tangu mwaka 2017.

Rais Magufuli aliwataka watendaji kuwajibika katika kufanikisha shughuli za uwekezaji ikiwemo wa viwanda kwa kuwa viongozi wa kisiasa unapokaribia uchaguzi wakati mwingine hawachangamkii mambo yenye faida kwa taifa.

CHAMA cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) kimekubaliwa ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi