loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC: Ondoeni vikwazo mkamilishe hospitali

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge, ameutaka uongozi wa Wilaya ya Chemba kuondoa vikwazo vidogo kama vile kuwa na mafundi wachache katika ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo ili ikamilike kwa wakati.

Aliyasema hayo juzi wakati akipotembelea ujenzi wa mradi huo wenye majengo saba ya utoaji huduma ya afya unaogharimu kiasi cha Sh bilioni 1.5 huku ukitarajiwa kukamilika Mei, mwaka huu.

Alisema uwepo wa mafundi wachache katika utekelezaji wa mradi utakwamisha mradi huo kutokamilika kwa muda uliopwanga na hivyo kuendelea kuchelewesha huduma za afya kwa wananchi.

“Vipo vikwazo vido vidogo ambavyo mnatakiwa kukaa meza moja na kuangalia namna ya kukabiliana navyo, mfano mnatakiwa kujua ni nini vinafanya maji na saruju kuchelewa, kwa nini mafundi wamekuwa wachache kwenye mradio huu,” alieleza.

Hata hivyo alimtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo Dk Semistatus Mashimba na timu yake, kuhakikisha wanaamkia katika eneo la mradi huo kila siku na si kumuachia mhandisi wa wilaya peke yake ili kila shughuli ifanyike kwa wakati uliopangwa. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo Simon Odunga alisema watakaa na mafundi hao ili kujua ni wapi wanakwama licha ya kuwa waliwahakikishia kuwa waliopo wanatosha.

“Nilipokuwa nikizungumza nao jana waliniambiwa mafundi waliopo wanatosha, na huu ukuta unaouona umejengwa kwa siku mbili yaani jana na leo na wakanihakikishia kuwa baada ya siku mbili nyingine watakuwa wamefikia hatua ya kufunga lenta lakini kwa maagizo hayo tutakaa nao ili waongeze mafundi wengine,” alisema Odunga.

Akizungumzia madai ya mafundi kutolipwa fedha zao Kaimu Mhandisi wa wilaya hiyo Filomena Bango alikanusha madai hayo akisema mafundi wote wakwishalipwa fedha zao katika awamu ya kwanza ya ujenzi ambayo imekwishakamilika. Alisema kwa sasa wapo kwenye awamu ya pili ya ujenzi na maalipo yake na yaendelea kufanya kulingana na taratibu za malipo.

IKIWA fomu moja ya kuomba ridhaa ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Chemba

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi