loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Wakulima wa alizeti tumieni mbinu asili’

WAKULIMA wa zao la alizeti nchini wameshauriwa kutumia mbinu za asili ili kukidhi vigezo vya kufi kia soko la kimataifa katika nchi za Ulaya na India.

Ushauri huo ulitolewa jana na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Happines Mgalula, wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini ya athari za mabadiliko ya tabianchi katika mnyororo wa thamani wa zao la alizeti iliyofanyika chini ya shirika la maendeleo la Uholanzi, SNV.

Mgalula, alisema wakulima wa zao hilo wanashauriwa kuzalisha kwa kutumia mbinu za asili ili kukidhi vigezo vya soko la kimataifa katika nchi za Ulaya na India. “Alizeti ni miongoni mwa mazao yaliyopewa kipaumbele kuzalishwa hapa nchini kutokana na umuhimu wake katika kuongeza upatikanaji wa mafuta ya kula ndani na nje ya nchi hivyo tutumie mbinu za asili katika kuzalisha zao hili,” alisema.

Alizitaja mbinu hizo kuwa ni kutumia mbolea za asili katika kupanda na mbegu bora pamoja na kutumia viuatilifu vinavyoshauriwa na wataalamu wa kilimo kwa kila eneo husika.

Alibainisha kuwa zao hilo limepewa kipaumbele kuzalishwa nchini kutokana na umhimu wa kuongeza mafuta ya kula ambapo linachangia asilimia 51 ya mafuta yote yanayozalishwa na asilimia 40 ya mafuta yote yanayotumiwa hapa. Aidha, alisema mahitaji ya mafuta ya kula kwa sasa nchini yanakadiriwa kuwa kati ya mita za ujazo 300,000 hadi 400,000 na kutokana na ongezeko la idadi ya watu mahitaji hayo yataendelea kuongezeka kila siku.

CHAMA cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) kimekubaliwa ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi