loader
Picha

OUT yashika nafasi ya 13 duniani, ya pili Afrika

CHUO Kikuu Huria nchini (OUT) kimeshika nafasi ya 13 kati ya vyuo vikuu huria 102 kwa ubora duniani na kwa Afrika kimeshika nafasi ya pili. Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Elifas Bisanda alisema hayo alipokuwa akizungumza na HabariLeo chuoni hapo juzi.

Profesa Bisanda alisema Februari, mwaka huu ilitolewa taarifa ya ubora wa vyuo vikuu huria duniani ambapo vipo vyuo vikuu huria 102 kati ya hivyo, OUT imeshika nafasi hiyo ya 13 kwa ubora. Aliongeza kuwa katika Afrika vyuo vikuu huria vipo tisa, chuo hicho nchini kimeshika nafasi ya pili kwa ubora na Chuo Kikuu Huria Afrika Kusini ndicho kilichoshika nafasi ya kwanza. Kwa mujibu wa Profesa Bisanda, katika vyuo vyote 49 vilivyopo nchini, OUT ni namba sita kwa ubora.

Kwa upande mwingine alielezea changamoto iliyopo katika chuo hicho kuwa ni Jumuiya ya Watanzania kutoelewa vizuri mfumo wa elimu masafa, wakifikiria kuwa ni elimu ya chini na hafifu. Alisema katika chuo hicho wanafunzi wanakuwa na uelewa mkubwa kwa kuwa hawafundishwi darasani lakini wanapewa maeneo yote ya kusoma ili wayapitie waweze kufanya vizuri katika mitihani yao. “Mtihani unatungwa kulingana na mtaala. Na ubora wa elimu inayotolewa chuoni hapa hauwezi kulinganishwa na vyuo vingine kwa kuwa mwanafunzi anasoma katika wigo mpana,” alisema.

Alisema hata wanafunzi wanaomaliza Kidato cha Sita hawaelewi ubora wa elimu unaotolewa na chuo hicho, hivyo wamekuwa wakifanya kampeni shuleni kwa ajili ya kuwaelimisha wanafunzi hao kujiunga na OUT. Mwaka jana chuo hicho kilikuwa na wanafunzi 8,000 lakini sasa wamefikia wanafunzi 12,994 na kabla ya kuondolewa kozi ya foundation mara ya kwanza na hatimaye kurudishwa chuo hicho kilikuwa na wanafunzi 16,000.

Mbunge wa Tandahimba, Katani Ahmed (CUF) amejiuzulu kiti ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi