loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

‘Mirembe haimaanishi kuwa Dodoma ina vichaa wengi’

HOSPITALI ya Rufaa ya taifa ya Mirembe haikujengwa mkoani Dodoma kutokana na mkoa huo kuwa na wagonjwa wengi wa akili (vichaa) bali kuwepo kwa gereza la Isanga ambalo wanafungwa wahalifu wakubwa na wauaji wanaotakiwa kupimwa akili zao.

Naibu Waziri wa Afya, Maendelelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile alitoa kauli hiyo baada ya Spika Job Ndugai kutaka kujua kama hospitali hiyo ya kutibu wagonjwa wa akili ilijengwa hapo kufuatia Dodoma kuwa na wagonjwa wengi wa akili.

Dk Ndugulile alisema hospitali hiyo ilijengwa hapo kutokana na Dodoma kuwa na gereza la Isanga lenye wafungwa wa mauaji na wahalifu wakubwa ambao hutakiwa kupimwa akili zao.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) aliyetaka kujua kwa nini dawa za kifafa na ugonjwa wa akili wilayani Ulanga mgao wake ni kidogo wakati wilaya hiyo inaongoza nchini kwa kuwa na wagonjwa wengi wa maradhi hayo. Dk Ndugulile alisema ni kweli Morogoro hasa wilaya ya Ulanga kuna wagonjwa wengi wa kifafa na akili, lakini atafuatilia kujua kwa nini dawa hizo hazifiki huko wakati zipo za kutosha.

Akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Njombe Mjini, Edward Mwalongo (CCM) aliyetaka kujua serikali inajipangaje kuwatibu, kuwapa mavazi na makazi wagonjwa wa akili mitaani. Dk Ndugulile alisema wizara inaendelea kuimarisha huduma za afya nchini ikiwemo huduma ya afya ya akili. Uimarishaji huo wa huduma ya afya ya akili unakwenda hadi ngazi ya afya ya msingi ambako ndiko jamii ilipo.

“Pamoja na kuongezeka kwa wagonjwa wa akili wanaorandaranda barabarani, sheria ya afya ya akili ya mwaka 2008 inawataka ndugu na jamii kuibua wagonjwa wa akili na kuwapeleka vituo vya kutolea huduma wapewe tiba,” alisema. Alisema wagonjwa wakipata nafuu, huruhiswa kukaa na familia zao na jamaa zao. Jukumu la kwanza la kulinda afya ya jamii huanzia ngazi ya familia, lakini jamii zinawanyanyapaa, kuwabagua, kuwatenga hivyo kuranda mitaani.

IKIWA fomu moja ya kuomba ridhaa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi