loader
Picha

ATCL inastahili pongezi

MOJA ya mashirika nyeti hapa nchini ni Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL). Mwaka 1977 ATCL ilikuwa na ndege tisa, lakini kutokana na usimamizi mbaya kampuni hiyo ilishindwa kuendelea kutoa kikamilifu huduma za usafiri.

Mwaka 1994 iliunganisha nguvu na kampuni za ndege za Uganda na Afrika Kusini, ambapo zilifanya kazi kwa miaka sita hadi mwaka 2000, ilipotangaza kupata hasara ya Sh bilioni 50.

Mwaka 2007 serikali ililichukua shirika hilo likiwa linasuasua.

Rais John Magufuli alipoingia madarakani mwaka 2015, moja ya ahadi zake ilikuwa ni kununua ndege mpya, jambo alilotekeleza na hadi sasa zimeshanunuliwa ndege sita ambazo ni Bombardier Q 400 tatu, Boeing 787-8 Dreamliner moja na Airbus A220-300 mbili.

Hivyo, tumevutiwa na habari katika gazeti hili juzi, iliyosema ‘ATCL kupasua anga la India’. Kwa mujibu wa habari hiyo, ATCL sasa imepewa kibali rasmi cha kuanza safari za ndege zake kwenda nchini India.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi anabainisha kuwa kibali hicho, kimetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa India. Matindi anashukuru kwa kupewa kibali hicho, lakini kwamba watatoa taarifa zaidi hapo baadaye.

Tunaipongeza ATCL kwa kupata kibali hicho, hasa kwa kuzingatia kuwa miezi michache iliyopita kampuni hiyo ilieleza kuwa imechelewa kuanza safari za nje ya nchi, kutokana na mambo ya msingi yaliyokuwa yakifanywa, mfano nchi kurudishwa katika Jumuiya ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (IATA).

Matindi anaeleza kuwa walipanga kuzindua mapema safari za nje, lakini walichelewa kwa sababu ya kukamilisha mambo ya msingi yaliyohitajiwa na IATA, ambayo kwa sasa wameshafikia mwisho.

Mbali na ruti hiyo ya India, ruti nyingine ambayo ATCL inatarajia kuanza kuihudumia karibuni ni China.

Imeelezwa kuwa ATCL itaanza safari za ndege mwezi Juni mwaka huu kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam hadi mjini Guangzhou, China, lengo likiwa ni kuinua biashara na utalii kati ya nchi hizo mbili.

Taarifa hiyo ilitolewa wiki iliyopita katika sherehe ya kuzindua Ofisi ya Uhusiano ya Ubalozi wa China nchini mjini Dodoma, ili kuitikia wito wa serikali kuhamia mjini humo. Kwa ujumla, ATCL inastahili pongezi nyingi kwa mafanikio hayo makubwa ambayo imeyapata. Yajayo yanafurahisha!.

HIVI karibuni wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake bungeni, Waziri ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi