loader
Picha

Mchekeshaji ashinda urais wa Ukraine kwa kishindo

Mchekeshaji maarufu nchini Ukraine, Volodymyr Zelenskiy (41) ameshinda nafasi ya Urais kwa asilimia 73.4 ya kura zote zilizopigwa dhidi ya mpinzani wake, Petro Poroshenko aliyekuwa akitumikia nafasi hiyo tangu mwaka 2014.

The Guardian la Uingereza linaripoti kuwa Zelenskiy ambaye hana uzoefu wowote katika siasa zaidi ya kuigiza nafasi ya urais katika vipindi vyake vya runinga.

Kutokana na matokeo yaliyotangazwa leo Jumatatu asubuhi (Aprili 22, 2019) ikiwa asilimia 85 ya kura zilizokwishahesabiwa, tayari zinazompa Zelensky nafasi ya kuwa Rais wa nchi hiyo.

Hata hivyo, amewashukuru wananchi wa Ukraine kwa kumuamini huku akisisitiza hayo yote yamefanyika kwa sababu ya umoja na mshikamano baina yao.

“Tumeshinda pamoja, nawashukuru wana Ukraine wote walionipigia kura na hata ambao hawakunipigia pia. Sitawaangusha,” alisema.

 Kwa upande  wa mshindani wake Rais Poroshenko amenukuliwa katika ukurasa wake wa Twitter akisema kuwa: “Ninaondoka Ikulu. Lakini nataka kuweka sawa kuwa kuondoka kwangu hakuniondoi katika siasa…nakubaliana na maamuzi waliyochukua raia wa Ukraine.”

 Poroshenko ametumikia nafasi ya Urais tangu mwaka 2014. Kabla ya hapo, amewahi kutumikia nyadhifa mbalimbali za kiserikali ikiwemo nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje tangu mwaka 2009 hadi 2010, na nafasi ya Waziri wa Biashara na Maendeleo ya uchumi mwaka 2012.

KILA mmoja ana njia yake ya kuonesha heshima ...

foto
Mwandishi: Mashirika

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi