loader
Picha

Yanga yatozwa faini mil. 3.5/-

YANGA imetozwa faini ya Sh 3,500,000 kutokana na makosa mawili tofauti huku beki wake Kelvin Yondani akifungiwa mechi tatu na faini ya Sh 500,000 baada ya kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar.

Adhabu hizo zilitangazwa jana baada ya Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi kukutana Aprili 18, mwaka huu na kupitia matukio mbalimbali.

Kwa mujibu wa adhabu hizo, Yanga ilitozwa Sh 3,000,000 baada ya kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi katika mechi dhidi ya Ndanda uliochezwa Aprili 4, mwaka huu, ikiwa ni mara ya nne wanafanya kosa linalojirudia.

Aidha, ilitozwa Sh 500,000 kutokana na mashabiki wake kuwarushia chupa za maji waamuzi wakati wakirejea vyumbani baada ya mechi hiyo kumalizika. “Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Klabu,”ilisema taarifa hiyo ya TFF.

Kwa upande mwingine, Yondani alifungiwa baada ya kumpiga ngumi mchezaji wa Kagera Sugar katika mechi dhidi yao iliyochezwa Aprili 11, mwaka huu Mwanza.

Kufungiwa kwake kutasababisha kukosa mechi zijazo mbili za ligi dhidi ya Azam FC na Tanzania Prisons na moja ya nusu fainali Kombe la Shirikisho la Azam (FA) dhidi ya Lipuli.

Wengine waliofungiwa kwa makosa yanayofanana na Yondani na kutozwa fainai sawa ni Aggrey Morris wa Azam FC, aliyempiga mchezaji wa Mbao katika mechi ya Aprili 7, mwaka huu, Paul Peter wa Azam aliyempiga ngumi mchezaji wa Mbeya City katika mechi ya Aprili 14, 2019 na Laurian Mpalile wa Tanzania Prisons aliyemkanyaga kwa makusudi mchezaji wa Mwadui katika mechi ya Aprili 3, mwaka huu.

Pia, klabu ya Ndanda SC imetozwa faini ya Sh 1,500,000 kwa kosa kama la Yanga ikiwa ni la kwanza msimu huu kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.

Meneja wa Kagera Sugar FC, Mohamed Hussein amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF baada ya kutolewa kwenye benchi la ufundi kwa kosa la kutoa lugha ya matusi kwa Mwamuzi katika mchezo huo uliochezwa

SERIKALI baada ya kufanya kikao na wadau wa michezo imesema ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi