loader
Picha

Nusu fainali Afcon leo

MECHI za nusu fainali ya Afcon kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, zinatarajiwa kupigwa leo Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ambapo mchezo wa mapema Guinea itacheza na Nigeria saa 10:00 jioni na mchezo wa pili Cameroon itachuana na Angola saa 1:00 usiku.

Mechi hizo mbili zinatarajiwa kuwa na upinzani mkali na washindi katika mechi hizo mbili ndio watakaocheza mechi ya fainali ambayo imepangwa kupigwa Jumapili Aprili 28, kwenye uwanja huo mkubwa wenye uwezo wa kubeba watazamaji 60,000.

Katika mchezo wa kwanza Guinea ambayo ni mshindi wa pili kutoka kundi B, inatarajiwa kutoa upinzani mkali kwa Nigeria waliomaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi A, kwa kujikusanyia pointi saba baada ya kushinda mechi mbili na sare moja.

Guinea hawapewi nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo kutokana na ubora wa Nigeria lakini vinara hao kutoka kundi A, wanapaswa kuwa makini kwani Guinea ni timu ambayo haitabiriki katika hatua ya makundi baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Cameroon ilionesha maajabu katika mechi zilizofuata na kuzifunga timu ngumu za Senegal na Morocco.

Katika nusu fainali ya pili Cameroon watakuwa na kibarua kipevu mbele ya Angola timu ambayo inaongozwa na mshambuliaji hata anayeongoza kwa mabao kwenye fainali hizo Osvaldo Capemba ambaye ana mabao matatu mpaka sasa.

Cameroon kama ilivyo Nigeria haijapoteza hata mchezo mmoja kwenye fainali hizo hivyo inakwenda kukutana na Angola.

SERIKALI baada ya kufanya kikao na wadau wa michezo imesema ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi