loader
Picha

7 wafungwa maisha kwa kuvamia meli

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewahukumu kifungo cha maisha jela raia saba wa Somalia baada ya kupatikana na hatia ya uharamia kwa kuvamia meli na kuipiga risasi.

Washitakiwa waliohukumiwa ni Mohammed Nuru, Bashir Rooble, Muhsin Haji, Abdulwaidi Abdallahamani, Farahani Abdul, Ally Ally na Omary Mohammed, ambao walikabiliwa na kosa la uharamia kinyume cha kifungu cha 66 (1)(a)(I) na (2) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.

Akisoma hukumu hiyo mwishoni mwa wiki, Jaji Yose Mlyambina alisema upande wa mashitaka ulileta mahakamani hapo mashahidi 14, na mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa.

Inadaiwa Oktoba 3, 2011 saa 1:30 usiku maeneo ya Bahari ya Hindi, maharamia hao walifanya uvamizi kwenye meli ya Sams All Good kwa kuipiga risasi hadi wanajeshi wa majini walipoweza kuiokoa boti ndogo aina ya Skiff iliyokuwa imevamiwa. Imeelezwa kuwa wanajeshi hao walifanikiwa kuwakamata na kuwafikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Pwani ambako upelelezi ulikamilika na washitakiwa kusomewa maelezo ya mashahidi.

Baadaye, Februari mwaka huu, kesi hiyo ilianza kusikilizwa Mahakama Kuu ambapo upande wa mashitaka katika kesi hiyo uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga, akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Cecilia Shelly na Wakili wa Serikali, George Barasa.

Washitakiwa waliwakilishwa mahakamani na Wakili Aloyce Komba, Domicus Mkwera, Rupia Abraham, Omary Msemo, Dennis Tumaini, Benedict Pius na Velasquez Severine. Kabla ya kutolewa adhabu, upande wa mashitaka uliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa washitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine. Hata hivyo, washitakiwa hao waliomba mahakama kuwapunguzia adhabu kwa sababu ni wakosaji wa kwanza na kwamba wanafamilia zinazowategemea.

MAKUBALIANO ya mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi