loader
Picha

Polisi Manyara yasaka wafungwa waliotoroka

POLISI mkoani Manyara inawasaka wafungwa wawili waliotoroka wakiwa chini ya ulinzi wa polisi wakati wakiwa wanasimamiwa kufanya kazi katika shughuli za ujenzi wa nyumba za polisi unaoendelea wilayani Babati.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Augustino Senga alithibitisha kutoroka kwa wafungwa hao Aprili 12, mwaka huu, saa 9:20 alasiri maeneo ya Bagara, Kata ya Bagara, Tarafa ya Babati wilayani humo. Kamanda Senga alisema wafungwa hao wenye namba 108/2019 Lekitambi Kambuu (28) wa Gereza la Babati na mwenzake namba 109/2019, Abirikaa Sokoine (25) walitoroka chini ya ulinzi wa polisi.

Alisema msako mkali unaendelea wa ufuatiliaji wa kuwabaini na kuwakamata wafungwa hao waliotoroka. Katika tukio jingine, lililotokea Aprili 15, mwaka huu, saa 7:00 mchana katika Kijiji cha Magara, Kata ya Magara Tarafa ya Mbugwe Wilaya ya Babati, mwanamke mkulima mkazi wa kijiji hicho, Regina Manday (35), aliuawa kwa kupigwa ngwala na kuangukia kisogo.

Kwa mujibu wa Senga, mtuhumiwa Claudi Swedi maarufu kwa jina la Claud Safari (35), mkulima na mkazi wa Kijiji cha Moya, amekamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria baada ya upelelezi kukamilika. Kamanda Senga alisema Manday alikwenda kulala kambini akiwa mfanyakazi kibarua wa shamba la Rift Wall Plantation inayomilikiwa na Riwa Ganji lililoko Magara, ambako akiwa anapita maeneo ya korongoni au mtoni ndipo alipopigwa ngwala na kuangukia kisogo na kufa.

Mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya maziko baada ya uchunguzi wa kitabibu. Aidha, alielezea mafanikio ya misako na doria mbalimbali zinazoendelea, imeliwezesha jeshi hilo kukamata dawa za kulevya aina ya bangi misokoto 1,248 na kete 24 kutoka katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

Katika geti la ukuta wa kuingia katika machimbo ya madini ya tanzanite yaliyopo Kata ya Mirerani wilayani Simanjiro, Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama wakati wa upekuzi wa kawaida wa kila siku walimkamata Jacob Ngoti (43), mfanyabiashara akiwa na misokoto 1,248 sawa na uzito wa kilo 2,740.

“Mtuhumiwa alitumia mbinu ya kuweka misokoto hiyo kwenye begi la nguo la mgongoni ili asiweze kugundulika kirahisi na chanzo cha tukio ni kujipatia kipato kutoka kwa wachimbaji ndani ya ukuta kwa kuwauzia dawa za kulevya kitendo ambacho hakitavumilika,” alisema Kamanda Senga.

MAKUBALIANO ya mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ...

foto
Mwandishi: Theddy Challe, Babati

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi