loader
Picha

Simba yaipumulia Azam

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Simba wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM, Kirumba Mwanza.

Mabao ya Simba yalifungwa na Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi.

Ushindi huo unawafanya wekundu hao kufikisha pointi 63 ikiikaribia Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwa pointi 66 katika michezo 32.

Simba ikishinda mchezo unaofuata dhidi ya KMC itafikisha pointi 66 sawa na Azam lakini itaishusha kwenye msimamo kutokana na kuwa na uwiano mzuri wa mabao.

Niyonzima aliiandikia Simba bao la uongozi dakika ya 20 baada ya kupokea pasi ya Mzamiru Yassin lililodumu kwa kipindi kizima cha kwanza.

Kipindi cha pili Simba ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Hassan Dilunga, Adam Salamba na John Bocco na kuingia Clatous Chama, Okwi na Meddie Kagere.

Mabadiliko hayo yalisaidia kuongeza kasi ya wekundu hao baada ya Okwi kuifungia timu yake bao la pili dakika ya 75 akiwachambua mabeki wa Alliance na kupiga shuti lililomshinda kipa wa timu hiyo.

Alliance walijaribu kuingia ndani ya eneo la Simba mara kadhaa na kushindwa kutumia nafasi walizotengeneza.

Kadhalika kwa wekundu hao, walipoteza nafasi kwa vipindi tofauti kutokana na kubanwa na mabeki wa timu pinzani.

Kitendo cha Alliance kupoteza kinazidi kuwaweka hatarini katika nafasi ya 16 ikikaribia mstari wa kushuka daraja baada ya kucheza michezo 33 na kujinyakulia jumla ya pointi 37.

SERIKALI baada ya kufanya kikao na wadau wa michezo imesema ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi