loader
Picha

Mwakyembe- Ahadi ziliwachanganya Serengeti Boys

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amelaumu ahadi zilizotolewa na mawakala kwa vijana wa Serengeti Boys na kusema ziliwachanganya kiasi cha kusababisha wafanye vibaya katika mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17, ‘Afcon’.

Akijibu hoja mbalimbali za wabunge jana kabla ya bajeti ya wizara yake kupitishwa, Mwakyembe alisema ameagiza Baraza la Michezo Tanzania (BMT) litengeneze kanuni za kuendesha shughuli za uwakala kwa vijana.

Awali, Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) amesema vijana hawakuandaliwa vizuri ndiyo maana hawakufanya vizuri.

“…Hapana, mpira ni mpira.Tuliwaandaa vizuri sana. Niulize swali, hawa vijana walichukua vikombe ‘competitive’ (vyenye ushindani) kama CECAFA na COSAFA kwa kubahatisha? Hapana. Ni kwa sababu ya mazoezi mazuri.”

Alisema katika mpira ni lazima mwingine ashindwe na mwingine ashinde. Hata hivyo alisema vijana walikuwa na presha kubwa ya kubeba matumaini ya watanzania wakati umri wao ni mdogo.

Akiendelea kueleza mambo yanayoweza kuchangia wakafanya vibaya tofauti na maandalizi mabaya, Dk Mwakyembe alisema “Lakini vile vile mimi nawalaumu mawakala; walikuja ‘ma agents’ kutoka nchi mbalimbali… kundi la Eto’o (Samuel Eto’o wa Cameroon) …unawaambia watoto wale tunakuhitaji tutakulipa milioni 100 kwa mwezi. Anachanganyikiwa, kanacheza pale kanaangalia ile hela.

Alisema, “Mimi nafikiri yametufundisha. Nimeiagiza BMT itengeneze kanuni kwa ajili ya kurejesha shughuli za uwakala hapa nchini kuhusu vijana wetu.”

SERIKALI baada ya kufanya kikao na wadau wa michezo imesema ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi, Doodma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi