loader
Picha

Namungo yatia timu Ligi Kuu

NAMUNGO FC ya Ruangwa, Lindi imekuwa timu ya kwanza kufuzu Ligi Kuu Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mawenzi Market kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

Namungo FC kwa matokeo ya mchezo huo imefikisha pointi 40 lakini uamuzi wa kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana kuipa ushindi dhidi ya Friends Rangers yameifanya kufikisha pointi 43 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine kwenye kundi lake A, huku ikiwa na michezo miwili kibondoni.

Mawenzi Market pia ilitumika kuwa daraja msimu uliopita, Februari mwaka 2018 ikicheza ligi daraja la kwanza uwanja wa nyumbani na kukubali kupokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Coastal Union ‘ Wagosi wa Kaya matokeo yaliyowapandisha Ligi Kuu.

Katika mchezo uliofanyika juzi Namungo FC walijipatia bao la kwanza katika dakika 31 lililofungwa na mchezaji wake Abeid Athuman kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa Reliants Lusajo na kuongeza bao la pili dakika ya 45 likifungwa na Lusajo kwa kichwa baada ya kupokea pasi ya mpira wa juu kutoka kwa mlinzi Miza Kristom.

Washambuliaji wa Mawenzi Market katika kipindi hicho walijaribu kufanya mashambulizi ya kushitukiza na kukosa nafasi kadhaa za kufunga mabao ikiwemo ya Joseph Mkoda (dakika ya 19) na Offen Chikola (dakika 21).

Kipindi cha pili, Mawenzi Market walizinduka na kujipatia bao dakika ya 46 kupitia kwa mchezaji wake Chikola baada ya kuwatoka mabeki wa Namungo FC na kupinga shuti kali lililomshinda kipa wa timu hiyo Adam Oseja na kujaa wavuni.

Zikiwa zimesalia dakika 20 mchezo huo kumalizika, Mwamuzi Bakari Shaweji wa Pwani alimwonyesha kadi nyekundu nahodha wa Namungo FC Hamisi Farhi kwa kumchezea vibaya mchezaji wa Mawenzi Seleman Kibadeni, awali beki huyo alikuwa na kadi ya njano.

Kihistoria, Namungo FC ikiwa hatua ya makundi ya mabingwa wa mikoa msimu uliopita kituo cha Morogoro ilipenya na kupanda ligi daraja la kwanza na msimu huu imeutumia vyema uwanja wa Jamhuri wa Morogoro na kutinga Ligi Kuu.

Timu nyingine zilizoutumia vyema Uwanja wa Jamhuri kwa kupanda Ligi Kuu kwa kuzifunga timu wenyeji mbali na timu hiyo, ni Coastal Union, Mbeya City katika msimu wa mwaka 2013/2014 na African Lyon msimu wake wa kwanza mwaka 2009/2010 ilipoifunga timu ya Jabal Hira ya Morogoro bao 1-0.

Kundi A lilikuwa na timu 12 mbali na zilizocheza siku hiyo nyingine ni Mlake FC, Maji Maji FC, Reha FC, Mbeya Kwanza, Mufundi United, Friends Rangers, Kiluvya United , Ashanti United, Njombe Mji FC na Dar City FC.

SERIKALI baada ya kufanya kikao na wadau wa michezo imesema ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi