loader
Picha

'Wake/waume wa wabunge wana haki VIP'

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amesema wenza wa wabunge wana haki ya kuhudumiwa kwa viwango vya VIP kwenye viwanja vya ndege nchini.

Amelazimika kutoa maelezo hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Nyang'hwale, Hussein Amar kwenye kipindi cha Maswali na Majibu bungeni leo, Jumatano.

“Wenza wa wabunge huwa wanapata huduma zote stahiki za VIP, hivyo kama kuna shida imewahi kutokea, basi ilikuwa sio ya kawaida,” aliongeza.

Kwa upande mwingine, Mhandisi Nditiye amesema maandalizi yameanza kwa ajili ya upanuzi wa uwanja cha ndege cha Arusha kwamba hivi karibuni mkandarasi ataanza kazi hiyo.

Ametoa ufafanuzi wa mradi huo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Catherine Magige aliyeuliza mpango wa serikali juu ya upanuzi wa uwanja huo ikizingatiwa kuwa ni sehemu yenye shughuli nyingi za kitalii.

MAKUBALIANO ya mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ...

foto
Mwandishi: Na JANETH MESOMAPYA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi