loader
Picha

Rais Magufuli aanza ziara Malawi

Rais John Magufuli amewasili Malawi kuanza ziara ya siku mbili.

Rais Magufuli ambaye ameongozana na mkewe, Mama Janeth Magufuli amepokelewa na mwenyeji wao, Rais Arthur Mutharika.

Wakati wa ziara hiyo Rais Magufuli anatarajiwa kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya aliyekuwa Rais wa Malawi Hayati Bingu Mutharika.

Baada ya hapo, Rais Magufuli atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Mutharika na baadaye kuhudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa maalumu kwa ajili yake.

Ratiba inaeleza kuwa baada ya tukio hilo, wawili hao watafungua msimu wa soko la tumbaku na kuzungumza na wadau.

Baada ya ziara hiyo, Rais Magufuli atarejea nchini na kuanza ziara ya kikazi ya siku nane mkoani Mbeya.

MAKUBALIANO ya mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ...

foto
Mwandishi: Na JANETH MESOMAPYA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi