loader
Picha

TMA yataja maeneo yatakayoathiriwa na kimbunga Kenneth

Kuanzia kesho Alhamisi, kimbunga kilichopewa jina la Kenneth kitakuwa umbali wa kilomita 150 kufika pwani ya Tanzania, Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) yangaza leo, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi, Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma za Ufundi wa TMA, Dk Pascal Waniha amesema kuwa kimbunga hicho chenye ukubwa wa 6/10 kinatarajiwa kuathiri mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na maeneo ya jirani.

“Kimbunga hicho kitakuwa cha kasi ya kilometa 100/saa na kitaathiri zaidi mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na maeneo ya jirani kwa takriban km 500,” amesema.

Ameongeza kuwa athari zinazotarajiwa ni pamoja na mafuriko, ongezeko la mvua kwa maeneo mengi, kuharibika kwa miundombinu na nyumba kuezuliwa mapaa.

Athari nyingine, kwa mujibu wa TMA, ni ongezeko la kina cha maji, kuathirika kwa shughuli nyingi za usafiri majini, nchi kavu na angani.

MAKUBALIANO ya mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ...

foto
Mwandishi: Na JANETH MESOMAPYA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi