loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Burundi yaifuata Tanzania SADC

SERIKALI ya Burundi imesema iko tayari kuungana na nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kwa kuwa imeshajipima na kujiona ina vigezo vyote vya kuwa mwanachama mpya.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Ezechiel Nibigira alimtembelea Mwenyekiti wa SADC, Rais wa Namibia, Hage Geingob na kueleza utayari wa taifa hilo la Afrika Mashariki, kujiunga SADC, jumuiya yenye nchi wanachama 16.

Kama itakidhi vigezo na kukubaliwa, Burundi itakuwa nchi ya pili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuwa mwanachama wa SADC, kwani kwa sasa iliyopo ni Tanzania pekee.

“Tumeweka mambo yetu sawa, sasa tunaikaribisha timu ya wataalamu wa SADC kuja kutukagua kuanzia mwezi ujao ili kuona kama tunakidhi vigezo au hapana. Lakini kwa upande wetu, tumejipanga na tuko tayari kwa uanachama wa SADC,” Nibigira alimweleza Rais Geingob.

Mwaka 2017 Burundi na Comoro ziliomba uanachama wa SADC, lakini Burundi ilichujwa wakati Comoro ikipitishwa kuwa mwanachama wa 16. Nibigira alisema tangu mwaka 2015, wamejitahidi kuondoa changamoto mbalimbali za kisiasa na sasa wako vizuri.

BARAZA jipya la mawaziri nchini Burundi, lililoteuliwa na Rais mpya, ...

foto
Mwandishi: BUJUMBURA, Burundi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi