loader
Picha

Hongera China kuwekeza mazao EAC

BIASHARA ya mazao ya Tanzania, Kenya na China imekuwa ikikua zaidi hivyo kutoa fursa kwa wakulima wa nchi hizi mbili za Afrika Mashariki kupata soko la uhakika.

Kwa Tanzania, zao la mihogo limeweza kupenya baada ya wafanyabiashara wa China kuamua kuwekeza katika viwanda vya kuchakata mihogo hapa nchini ambapo wakulima watanufaika kwa kiasi kikubwa.

Kama ilivyo kwa zao la muhogo hapa nchini, wiki iliyopita jijini Beijing, China, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mwenzake wa China, Xi Jinping walitia saini uwekezaji wa zao la parachichi.

Hizi ni habari njema kwa nchi hizi mbili za Afrika Mashariki kwa kuwa kati ya tatizo ambalo limekuwa likizidisha umasikini, ni wakulima kukosa soko la uhakika kwa mazao walimayo.

Tunawapongeza marais, Jinping na Kenyatta kufanikisha nchi hizi kuingia kwenye mauzo hayo ya zao la parachichi kutokana na kuzalishwa kwa wingi Kenya. Hii ni fursa nzuri kwa wakulima wa Kenya kuzalisha maparachichi bora yanayoweza kuleta ushindani mkubwa katika soko la dunia.

Kenya ni miongoni mwa nchi zinazozalisha maparachichi kwa wingi katika nchi za Afrika Mashariki.

Makubaliano hayo yatawawezesha wakulima wa Kenya kusafirisha parachichi kwenda China, ikiwa ni fursa kutangaza bidhaa zinazozalishwa Kenya ambazo hazina uwekezaji wa kimataifa.

Kama ilivyo kwa zao la muhogo kwa wakulima Watanzania, wakulima parachichi nchini Kenya watumie nafasi hii adhimu kulima kwa wingi ili wao wafaidi lakini pia nchi ipate fedha za kigeni.

Tuzishauri nchi nyingine za Afrika Mashariki kutafuta mazao ambayo yanalimwa kwa wingi katika nchi zao na kuyatafutia soko la uhakika.

Wizara zinazoshughulikia kilimo zitafute masoko ya uhakika kwa wakulima wa mazao hayo yanayopatikana katika nchi zao kwa kuwa mbali na kuwanufaisha, pia nchi zinapata fedha za kigeni.

Uchumi wa nchi unategemea pia mtu mmoja mmoja, hivyo tunazishauri wizara za kilimo kutafuta masoko ya mazao husika ili wakulima waweze kupata kipato cha uhakika.

Tunawapongeza pia wafanyabiashara wa China kwa kukubali kuwekeza katika mazao haya mawili ingawa tunaamini, bado kuna nafasi kubwa katika mazao mengine katika nchi za Afrika Mashariki ambayo yanahitaji uwekezaji.

Yapo mazao kama mahindi, mtama, uwele na mengineyo mengi na pia nchi za Afrika Mashariki zimejaliwa kuwa na matunda ya aina mbalimbali ambayo yanahitaji uwekezaji mkubwa.

MCHUMI kutoka Chuo Kikuu cha Oxford cha Uingereza, Profesa Christopher ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi