loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watendaji wazembe hawamtendei haki Magufuli

PAMOJA na viongozi wengi wa serikali kufanya kazi kama ambavyo wamekuwa wakielekezwa na Rais John Magufuli wakati wa uteuzi wao, wapo wachache ambao wameziba masikio kwa makusudi na hivyo kuendelea kumchefua Rais.

Tabia hii imekuwa si tu inakera bali pia inatia doa na inarudisha nyuma nia na malengo mazuri ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Akioneshwa kukerwa na utitiri wa mabango ya wananchi kwenye kila ziara na mikutano anayofanya mikoani, ukiwamo Mkoa wa Mbeya, Rais Magufuli jana aliwataka wasaidizi wake wakiwamo mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi, maofisa tarafa, vijiji na wabunge, kutenga muda wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Hili ni agizo ambalo naamini kila mwenye mamlaka katika eneo lake la kazi hanabudi kulifanyia kazi haraka ili kuendana na matakwa ya Rais Magufuli ambaye amejitoa kuwatetea wanyonge.

Viongozi wa ngazi zote wanawajibika kwa wananchi kama Rais anavyowajibika kwao, hivyo haiingii akilini kuona wananchi wanabeba mabango ili kero zao ambazo zingekuwa zimetatuliwa na viongozi wa ngazi mbalimbali lakini zikaachwa hadi Rais anapotembelea maeneo yao.

Hii ni kero kubwa.

Ni kubwa kwa sababu, kila mmoja akitimiza wajibu wake, hakuna haja ya Rais Magufuli kukumbana na mabango kwa kuwa watakuwa tayari wamepewa majibu na watendaji wengine kuanzia ngazi ya viongozi wa vitongoji, kata, tarafa, wilaya, mkoa hadi taifa.

Kutokana na viongozi kutowajibika, ndiko kunakosababisha wananchi kusubiri mkombozi wao ambaye amejitoa kuwatetea wanyonge.

Suala la uongozi ambao ninaamini ni wito, linahitaji kujitoa. Linahitaji moyo wa kujituma kwelikweli na pia kutanguliza maslahi ya wengi.

Tatizo la baadhi ya viongozi sio wote, wamebebwa na tamaa na ubinafsi, wameacha mambo ya wananchi wanaowatumikia na ndio maana wengi wanatimiza wajibu kwa kutaka kumfurahisha Rais au watendaji wao wakuu wanapowatembelea.

Ni kutokana na kutotimiza wajibu, Rais Magufuli amekuwa akipokewa na mabango kwa kuwa hakuna njia nyingine ya wananchi hao kufikisha matatizo yao yakapokelewa na kufanyiwa kazi.

Wanasheria wana msemo kwamba suala si kutoa haki bali ni kuona haki inatendeka. Watendaji wa serikali sio kazi kusikiliza kero tu bali ni kuzitatua, hivyo hata kama watatenga siku na kusikiliza kwa maagizo ya Rais, kama shida za wananchi hazitatuliwi ugonjwa utabaki pale pale.

Kero hizi ndogo na kubwa ambazo wananchi wanaziibua kwenye mikutano ya Rais John Magufuli, zimekuwa kweli zinamchukiza kutokana na wasaidizi wake kushindwa kuzitatua.

Akiwa wilayani Rungwe jana katika kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha Ualimu cha Mpuguso, wananchi wengi walionekana kubeba mabango huku maofisa usalama wakijaribu kuwazuia wasiyanyooshe, ndipo Rais Magufuli alipowaagiza askari hao wawaache wananchi hao kwa kuwa mabango hayo ni yake yeye.

MOJA ya shabaha ya kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ...

foto
Mwandishi: Bantulaki Bilango

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi