loader
Picha

Bakwata iheshimiwe kuandama mwezi

LEO au kesho Waislamu wanatarajia nyakati za Magharibi kuangazia angani, kuangalia kama mwezi umeandama, ili waweze kuanza kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, unaotarajiwa kuanza kesho au keshokutwa.

Ni mwezi wa toba, ambapo inatarajiwa waumini wa dini hiyo, watautumia kwa ajili ya kufanya ibada sana, lakini pia kutekeleza nguzo ya nne kati ya nguzo tano za dini hiyo, inayomtaka kila Muislamu mwenye afya njema, kufunga mwezi huu mtukufu unaoheshimika duniani kote.

Kwa mujibu wa dini ya Kiislamu, yeyote muadilifu anayeuona mwezi umeandama, anaweza kutoa taarifa na kufunga, lakini inatakiwa mamlaka ya dini ya nchi husika, ndiyo itangaze kuonekana kwa mwezi huo ili waumini wasipate mkanganyiko na waweze kufunga kwa pamoja.

Katika miaka ya nyuma, tumeona taarifa za kuandama mwezi wakati mwingine zikichelewa au taasisi tofauti za dini hiyo kutangaza tofauti, matokeo yake siku ya kuanza kufunga Waislamu wengine kujikuta hawakufunga kwa sababu ya kukosa taarifa.

Hali hii imekuwa ikilalamikiwa sana, kwani wengine wanasema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) halijaona mwezi, lakini watu wengine wameona mwezi na kuanza kufunga.

Ili kuondokana na mkanganyiko huu, Bakwata limeunda Kamati ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambapo Mufi wa Tanzania, Shehe Mkuu Abubakar Zubeir ameitangaza kamati hiyo na kwenda mbali zaidi kwa kutoa namba za simu O717 929057 ya Mufti, 0713247724 ya Shehe Alhad Mussa Salum na 0784246400 ya Shehe Abdallah Mnyasi, 0658267370 ya Shehe Hamid Jongo na 0655730430 ya Shehe Ali Mkoyogole.

Lengo la kufanya hivyo ni kuwataka mashehe na waumini wote wa dini ya Kiislamu nchini, kutoa taarifa za kuonekana kwa mwezi huo ili kamati ithibitishe na kisha wananchi kutangaziwa kuanza kufunga.

Sisi tunaipongeza Bakwata kwa hatua hii nzuri, kwani imejiweka wazi na karibu zaidi na waumini wake katika kusaidiana kuuona muandamo wa mwezi na kuwafanya wananchi waweze kufunga kwa pamoja na kuondokana na mkanganyiko na malalamiko yasiyo na sababu ya msingi.

Waislamu wote ni wamoja, hivyo kwenye mwezi huu inatakiwa kuwa kitu kimoja katika kufanikisha funga ya mwezi huu muhimu kwa waumini.

Tunawataka pia waumini wa Kiislamu, kuupokea mwezi huu kwa furaha ili waweze kuiona pepo kama Mtume Muhammad (S.A.W) alivyosema kwenye maandiko yake ya dini ya Kiislamu.

Mtume Muhammad (S.A.W) amesema kuwa mwezi huu ni wa Allah (S.W.T) na umewafikia watu pamoja na baraka, rehema na misamaha yake, kwani ni mwezi ulio bora, usiku na mchana wake ni bora kuliko usiku na mchana wowote mwingine, saa zake ndizo bora kabisa kuliko saa zote na ni mwezi ambamo Allah (S.W.T) anakubali na kuzijibu ibada na dua za waumini.

Kutokana na kauli hiyo ya Kiongozi wa Waislamu, tunawasihi waumini kufanya ibada na kubadilika kwa kuachana na matendo maovu.

Mwezi huu utumike kuwabadilisha Waislamu kwa kuacha dhuluma, ufisadi na matendo mengine yasiyofaa kwenye jamii. Wafanyabiashara nao tunawasihi kuacha tamaa kwa kupandisha bidhaa bei, bali wauze kwa bei halali na ikiwezekana washushe

MCHUMI kutoka Chuo Kikuu cha Oxford cha Uingereza, Profesa Christopher ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi