loader
Picha

Tuendelee kuchapa kazi kwa bidii

WIKI iliyopita wafanyakazi wa Tanzania, waliungana na wenzao duniani, kusherehekea Siku ya Wafanyakazi, maarufu Mei Mosi. Hiyo ni siku ambayo dunia huitumia kuenzi na kutambua mchango unaotolewa na wafanyakazi katika kuleta maendeleo.

Tunawapongeza wafanyakazi wote wa Tanzania kwa kuungana na wenzao duniani, kuadhimisha siku hiyo muhimu na pia kwa mchango wao mkubwa, wanaoutoa katika kuiletea maendeleo ya nchi yetu.

Pia, tunampongeza Rais John Magufuli kwa kuwahakikishia wafanyakazi kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao na kushughulikia changamoto zao mbalimbali.

Anawataka wavute subira na kuendelea kuchapa kazi kwa bidii ili kuiletea nchi yetu maendeleo, kama Serikali ya Awamu wa Tano inavyosisitiza kuwa “Hapa Kazi tu”.

Rais anasema anashukuru Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) kupitia risala yao, kwa kuipongeza serikali, kwa hatua mbalimbali ambazo serikali inachukua katika kujenga miundombinu na kuboresha huduma za jamii.

Kwa mujibu wa Rais, serikali imepokea risala hiyo na inaahidi kuwa yote yaliyomo kwenye risala, itayafanyia kazi.

Aidha, tunampongeza Rais jinsi kwa kuzungumzia kwa undani masuala yaliyomo kwenye risala hiyo na kuyatolea ufafanuzi.

Kwa mujibu wa Rais, masuala hayo ni maombi ya kutaka Bodi za Mishahara kukutana, kupunguza viwango vya kodi kwa watumishi wote, suala la watumishi wa darasa la saba na uboreshaji wa mazingira na usalama sehemu za kazi.

Kuhusu Bodi za Mishahara, Rais anafafanua kuwa hana tatizo na bodi hizo kukutana; na kwamba haielewi ni kwa nini hazikutani.

Hivyo, anaagiza waziri mwenye dhamana, kuhakikisha bodi hizo zinakutana, lakini kwamba vikao vyao, visiwe kichochoro cha kutumia vibaya fedha za serikali.

Kwa upande wa uboreshaji wa mazingira na usalama sehemu za kazi, anatoa mwito kwa waajiri wote kuzingatia sheria za kazi, ikiwemo Sheria ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi.

Kwamba waajiri hawana budi kutekeleza matakwa mengine ya kisheria, ikiwamo kutoa mikataba ya ajira na pia kuruhusu uwepo wa vyama vya wafanyakazi sehemu zao za kazi.

Aidha, anasema hana tatizo na suala la kupunguza viwango vya kodi. Rais anasema kama serikali iliweza kushusha kodi kutoka asilimia 11 hadi asilimia 9 kwa watumishi wa kima cha chini; bado inaweza kuendelea kujadiliana kwa ngazi nyingine.

RAIS John Maguful amemaliza ziara yake mkoani Katavi kwa kuzindua ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi