loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

NIDA Ubungo jipangeni

KAMA kawaida ya Watanzania hawawezi kufanya jambo lililotangazwa na serikali ambalo lina faida na maendeleo kwa wakati, badala yake wanasubiria mwishoni au muda wa nyongeza ndipo wafanye waliyoagizwa.

Hii ilijionesha katika mambo mbalimbali yaliyokwisha kutangazwa na serikali ikiwemo kujiandikisha kupiga kura na hata suala la kujiandikisha kupata vitambulisho vya taifa.

Kwa upande wa vitambulisho vya taifa, suala hili lilitangazwa muda mrefu sana. Baada ya kutangazwa kwamba uandikishaji wa vitambulisho hivyo utaishia Desemba, watu walijitokeza kwa wingi wakati kipindi cha katikati hawakuwa na mwamko wa kujiandikisha.

Kutokana na huruma ya serikali, iliamua sasa kwamba uandikishaji wa vitambulisho hivyo uwe endelevu kwa ajili ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata kitambulisho hicho.

Kwa sasa vitambulisho hivi ni muhimu sana kwani ili kumuwekea mtu dhamana mahakamani au polisi lazima uwe na kitambulisho hicho.

Kwa wale wanaohitaji mafao yao ya kazi na wenyewe hawawezi kupewa stahiki zao bila kitambulisho hicho. Ikumbukwe kuwa hivi karibuni kulikuwa na ujumbe mfupi wa maandishi ambao kila anayetumia simu nina uhakika ameupata na ulikuwa unasema ‘Ndugu mteja kuanzia terehe 1 Mei unatakiwa kusajili upya laini yako kwa mfumo wa alama za vidole.

Tembelea duka letu na kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA’. Baada ya ujumbe huo, watu wengi walianza kujitokeza kwenye ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na kuanza hatua za kujiandikisha.

Kama kawaida, mahitaji ya NIDA ili kujiandikisha kupata vitambulisho hivyo ni kuwa na barua kutoka serikali za mitaa, cheti cha kuzaliwa, nakala ya kitambulisho cha kupigia kura au leseni au hati ya kusafiria, cheti cha darasa la saba au kidato cha nne na kujaza fomu 1A ya mamlaka hiyo.

Mtu ambaye hana cheti cha kuzaliwa na kwamba alizaliwa miaka ya 1980, analazimika kwenda mahakamani kuapa na kiapo hicho kitatumika kama kielelezo cha kupata kitambulisho lakini wale waliozaliwa kuanzia mwaka 1990 anatakiwa kuwa na cheti hicho.

Pamoja na msururu wa watu wanaojiandikisha, wanaofuata vitambulisho hivyo ambavyo baada ya kujiandikisha hutoka kwa miezi mitatu, ni habari nyingine. Ofisi ya NIDA Wilaya ya Ubungo, ni miongoni mwa ofisi zinazopokea watu wengi wanaojiandikisha na kuchukua vitambulisho vya taifa hivi sasa.

Baada ya kuwepo kwa watu wengi kwa upande wa wanaojiandikisha waliamua kuweka mashine tatu za kupigia picha ili kurahisisha uandikishaji.

Lakini bado kuna changamoto kubwa kwa upande wa watu wanaochukua vitambulisho kwa sababu pamoja na kujiandikisha majina na tarehe ya kuzaliwa, maofisa wanapokwenda kuangalia kwenye mtandao kuna majibu ambayo wakati mwingine yanakatisha tamaa.

Wapo baadhi ya watu ambao wanaambiwa kuanza upya hatua za uandikishaji wa vitambulisho hivyo kwa sababu hawaonekani kwenye mtandao wao, wengine wanatakiwa kurudi tena ofisini hapo baada ya mwezi kwa sababu vitambulisho havijafika ofisini na vingine havionekani.

Kinachosikitisha ni kwamba maofisa hao licha ya kujua changamoto hizo wamekuwa na majibu ambayo kwa watumishi wa umma hawapaswi kuwajibu wananchi.

Natambua kwamba huu ni wakati wa presha kwa maofisa hawa wa NIDA kwani kila mtu anataka kitambulisho kwa ajili ya kukamilisha usajili ambao ni hadi Desemba mwaka huu, lakini wawe na uvumilivu hata wanapowajibu watu.

Naamka asubuhi,  sioni kilongalonga, 
Napapasa kitandani,  hamadi hiki hapa,  

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi