loader
Picha

Mwanafunzi aliwa na mamba akitoka shule

MWANAFUNZI wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Samazi iliyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Kalambo katika Mkoa wa Rukwa, Theresia George (11) amevamiwa na kuliwa na mamba wakati akivuka Mto Liwazi wakati akitoka shuleni.

Theresia ambaye ni mkazi wa kijiji cha Katili alilazimika kuvuka Mto Liwazi kwa kuogelea baada ya mtumbwi wa kijiji ambao ulikuwa ukitumika kuwavusha wananchi na wanafunzi katika Mto Liwazi kuharibika.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, Said Athanas amethibitisha kutokea kwa mkasa huo juzi na kuutaka uongozi wa kijiji cha Katili kuona uwezekanao wa kuwa na mitumbwi miwili ya kuwavusha wananchi na wanafunzi wakati serikali ikitafakari kukabiliana na changamoto hiyo. “Nimepokea taarifa za tukio hili kwa mshtuko mkubwa, nawaasa wazazi na walezi wasiwaache watoto wao kwenda peke yao na kuogelea mtoni au wanafunzi kuvuka kwa kuogolea wanapokwenda na kutoka shuleni kwa kuwa kuna mamba wengi,”alisisitiza.

Mkazi wa kijiji cha Katili, Juma Kilongwe alieleza kuwa mtumbwi ambao ni mali ya kijiji uliokuwa ukiwavusha wanafunzi na wananchi katika mto huo hautumiki tena baada ya kutoboka, hivyo wanafunzi wanalazika kuvuka kwa kuogelea wanapokwenda shule na kurudi nyumbani. Wakisimulia mkasa huo, mashuhuda kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini walidai kuwa siku hiyo ya tukio mwanafunzi huyo (Theresia) alivuka mto Liwazi hadi ng’ambo ya pili salama huku akiwa ameshikilia nguo zake mikononi.

“Lakini alipofanikiwa kuvuka salama hadi upande wa pili yaani kijijini Katili wanafunzi wenzake aliowaacha upande mwingine walimuomba arudi awachukulie nguo zao ili nao waweze kuvuka ...alifanya hivyo lakini alipojaribu kuvuka kwa mara nyingine na wenzake mamba mkubwa aliibuka ghafla na kumshambulia na kumvuta ndani ya maji,” alisema. Ofisa Mtendaji Kata ya Samazi, Pius Kasonso alithibitisha kuwa mwili wa mwanafunzi huyo haujaonekana licha ya wananachi kuutafuta kutwa nzima mtoni hapo.

MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020 utarejea tena Juni ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Kalambo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi