loader
Picha

Simba, Yanga gonjwa moja

WATANI wa jadi, Simba na Yanga hawachekani baada ya jana kupoteza mechi zao za Ligi Kuu Bara zilizochezwa kwenye viwanja tofauti. Mabingwa watetezi Simba wakiwa nyumbani uwanja wa Uhuru, walipoteza mechi dhidi ya Kagera Sugar kwa bao 1-0 na hivyo kutoa pointi sita kwa Kagera baada ya kufungwa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza.

Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jnr’wa Simba aliibeba Kagera Sugar kwa bao la kujifunga dakika ya 41 akiwa kwenye harakati za kuokoa mpira wa krosi wa David Luhende. Mpira huo wa kona ulipomfikia Zimbwe aliutuliza lakini kutokana na mawasiliano hafifu na kipa wale Aishi Manula aliyetoka golini kuufuta, alijikuta akipishana nao.

Safu ya ushambuliaji ya Simba ilifanya mashambulizi ya mara kwa mara kupitia kwa wachezaji wake Emmanuel Okwi, Hassan Dilunga na Meddie Kagere lakini beki ya Kagera ilikuwa makini kuondosha hatari langoni mwake. Kwenye uwanja wa Karume Musoma, bao la Tarif Seif liliizamisha Yanga dhidi ya Biashara United iliyoibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mchezo huo wa raundi ya 35 uliaza kwa kutawaliwa na matumizi ya nguvu kwa timu zote mbili hali iliyosababisha wachezaji kuanguka mara kwa mara. Shambulizi la dakika ya 09 lilofanywa na wenyeji Biashara liliwapa bao la uongozi kupitia kwa walifanikiwa kupata bao la uongozi kupitia kwa mshambuliaji wao Seif baada ya kupokea pasi ya mpira wa adhabu ndogo iliyozagaa kwenye eneo la hatari na kuwazidi ujanja safu ya ulinzi ya Yanga kabla ya kuachia chuti kali lilomshinda mlindamlango Clatous Kindoki na mpira kujaa wavuni.

Matokeo hayo yanafanya msimamo kubaki kama ulivyo kwa timu mbili za juu, Simba ikiongoza kwa tofauti ya pointi moja ikiwa na pointi 81. Kwa biashara matokeo yamekuwa na maana kubwa kwao kwani hawapo salama sana wakiwa nafasi ya 17 na kufikisha pointi 40. Kagera Sugar imefikisha pointi 43 ikisogea mpaka nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

foto
Mwandishi: Grace Mkojera na Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi