loader
Picha

Azam yaitibulia Simba

SIMBA jana ilitoka suluhu na Azam katika mechi ya Ligi Kuu Bara na hivyo kuifanya kusubiri zaidi kabla ya kupata pointi za kutosha kutetea taji lake. Mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam ilikuwa ya kuvutia huku timu zote zikishambuliana kwa zamu.

Matokeo hayo yanaifanya Simba iendelee kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 82, wakihitaji pointi nane kutangaza ubingwa. Kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo huo kutategemea na matokeo ya Yanga itakayocheza na Ruvu Shooting leo. Yanga ina pointi 80, ikishinda leo itaishusha Simba kwa tofauti ya pointi moja na hivyo kuongeza presha katika mbio za ubingwa.

Kwa upande wa Azam ambayo mechi yake ya kwanza na Simba ilifungwa mabao 3-0, imeendelea kubakia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 69. Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi alikosa mabao hasa katika kipindi cha kwanza ambapo ama alipiga juu, mpira kwenda nje au kuokolewa na mabeki wa Azam.

Mchezaji mwingine wa Simba aliyekosa mabao ni Clatous Chama, katika dakika ya 73 baada ya kushindwa kumalizia mpira uliokuwa ukielekea golini. Kwa upande wa Azam, Ngoma alishindwa kufunga dakika ya 77 akiwa na kipa Aishi Manula lakini alipiga mpira nje. Mechi nyingine iliyocheza jana katika ligi hiyo, Prisons ilishindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani Sokoine Mbeya baada ya kufungwa bao 1-0 na KMC. Katika mechi ya leo, Yanga inahitaji ushindi ili kufuta makosa katika mechi iliyopita ambapo ilifungwa na Biashara United.

NAHOD HA wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi