loader
Picha

Ubingwa wampa jeuri Guardiola

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema ushindi ni `tabia’ baada ya timu yake kutetea taji la Ligi Kuu, licha ya ushindani mkubwa kutoka kwa Liverpool.

Man City imekuwa timu ya kwanza ndani ya muongo mmoja kutetea taji la Ligi Kuu ya England, baada ya kutoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Brighton juzi na kuipiku Liverpool katika mbio hizo za ubingwa.

Man City iko mbioni kukamilisha kutwaa mataji matatu katika soka la Uingereza ndani ya msimu mmoja, endapo mwishoni mwa wiki itatwaa taji la FA katika mchezo wa fainali dhidi ya Watford. Katika mchezo huo wa mwishoni mwa wiki iliyopita, mabao ya Man City yalifungwa na Sergio Aguero, Aymeric Laporte, Riyad Mahrez na Ilkay Gundogan, huku lile la wenyeji likiwekwa kimiani na Glenn Murray.

“Ushindi ni tabia na ndani ya siku chache zijazo tutakuwa na Kombe la FA,” alitamba Guardiola. Ushindi wa michezo 14 mfululizo ya ligi kwa Guardiola juzi ulizima ndoto za muda mrefu za Liverpool kutwaa taji la Ligi Kuu, ambalo kwa mara ya mwisho walilibeba mwaka 1990 licha ya kushinda 2-0 dhidi ya Wolves katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Anfield.

Pia Man City ilishuhudia ikimaliza ikiwa na pointi nyingi za tatu katika historia ya Ligi Kuu baada ya kufikisha 98. Guardiola alielezea kuwa kutwaa taji la Ligi Kuu la msimu huu kama kitu kigumu zaidi katika Ligi Kuu nane akiwa kama kocha.

“Tulishinda Hispania na Ujerumani, lakini hii ni ngumu,” alisema Guardiola, ambaye ameshinda mataji matatu akiwa na Barcelona na Bayern Munich. “Ligi hii, makocha bora wako hapa, kuna wachezaji wazuri, hasa hawa wapinzani wetu tulikabiliana nao msimu huu.”

Kwa sekunde 83 baada ya Brighton kutangulia kufunga mashabiki wa Liverpool walianza kuota ubingwa, lakini Man City walidhihirisha kwa nini ni mabingwa baada ya kufikisha pointi 98, mbili pungufu ya rekodi waliyoweka msimu uliopita baada ya kufikisha pointi 100. “Tunatakiwa kuishukuru Liverpool kwa sababu wametusaidia sana kuwa bora kuliko hata msimu uliopita,” alisema Guardiola.

UONGOZI wa klabu ya Chelsea umempa ruhusa kiungo wake N’golo ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi