loader
Picha

Tari ilivyojipanga kuchochea uchumi wa viwanda

KATIKA kufi kia uchumi wa kati unaotegemea viwanda, uboreshaji wa kilimo chetu ni suala muhimu. Hii ni kwa sababu, mbali ya kutegemewa kuwalisha Watanzania wanaoongezeka kwa idadi mwaka hadi mwaka, kilimo kinategemewa pia katika kutoa sehemu kubwa ya malighafi kwa ajili ya viwanda hivyo.

Je, kilimo chetu kiko tayari kwa hilo? Jibu ni kwamba, kinapaswa kupiga hatua zaidi kuliko ilivyo sasa na kitu muhimu kitakachokinyanyua zaidi ni matumizi ya teknolojia na utafiti. Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari) inayojihusisha na usambazaji wa teknolojia mbinu na utaalamu wa kilimo wa kisasa kwa wakulima na wadau wengine, ni chombo chenye jukumu hilo adhimu la kukuza kilimo nchini.

Je, Tari ni nini, imetokea wapi na inafanya nini? Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo nchini, Dk Geoffrey Mkamilo anasema katika mazungumzo na mwandishi wa makala haya kuwa, Tari ilianzishwa kwa Sheria Namba 10 ya Mwaka 2016 iliyopitishwa na Bunge, ikipewa jukumu la kutafiti, kusimamia na kuhamasisha matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wakulima na wadau wengine.

Tari pia ina dhima ya ku- ratibu shughuli zote za utafiti wa kilimo Tanzania Bara. Idara kuu tatu Dk Mkamilo anasema Tari ina Idara kuu tatu am- bazo ni: Utafiti na Ubunifu; Usambazaji wa Teknolojia na Uhusiano pamoja na Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu.

“Shughuli zote za utafiti zinafanywa na Idara ya Utafiti na Ubunifu, anasema. Anasema Idara ya Usambazaji wa Teknolojia na Uhusiano ina jukumu la kuhakikisha teknolojia zote, ubunifu na mbinu bora za kilimo katika mazao yote ya kimkakati zinasambazwa ili kuwafikia wakulima na wadau wengine walioko katika mnyororo wa thamani. Aidha, anasema idara hiyo inahusika katika kuimarisha ushirikiano na wadau wa kilimo wa ndani, kikanda pamoja na wa kimataifa katika mnyororo wa thamani.

Vituo 18 vya utafiti Dk Mkamilo anasema kwa sasa kuna vituo 18 vya utafiti nchini. Anasema kila kituo kina jukumu la kitaifa la kufanya utafiti na maendeleo ya zao moja au zaidi ya moja. “Kila kituo cha utafiti,” Dk Mkamilo anasema: “Kinasimamia zao fulani ikiwa ni pamoja na kufanya utafiti na kisha kusambaza matokeo ya utafiti huo kwa wakulima.”

Vituo katika ikolojia Akizungumzia kituo cha Tari kilichoko Kibaha mkoani Pwani, anasema kimejikita zaidi katika utafiti na uendelezaji wa zao la miwa. Kwa mujibu wa Dk Mkamilo, mahitaji ya sukari nchini ni karibu tani laki tano kwa mwaka kwa sasa, lakini kiwango cha sukari inayozalishwa ni tani laki tatu tu kwa mwaka. Wao kama taasisi ya utafiti, anasema wanaangalia ni utalaamu, teknolojia na mbinu gani zitakazoongeza tija katika kilimo cha miwa na hivyo, kuongeza maradufu uzalishaji wa sukari nchini.

Vile vile, Dk Mkamilo anasema taasisi hiyo yenye makao yake Mikocheni, Dar es Salaam, inashughulikia utafiti wa zao la minazi na bayoteknolojia. Kwa upande wa Kituo cha Tari Mlingano kilichopo Tanga, anasema kina majuku- mu ya kutafiti zao la mkonge pamoja na utafiti wa udongo na matumizi ya mbolea. “Tanga kuna maabara kubwa ya kuangalia udongo nchi nzima ili kutoa mapendekezo kwa wakulima kabla ya kupanda mazao yao mbalimbali,” anasema.

Taasisi nyingine ni za Ifakara na Dakawa-Mvomero zilizopo mkoani Morogoro zinazoshirikiana kufanya utafiti wa zao la mpunga. Kwa maelezo ya Dk Mkamilo, Tari Ilonga wilayani Kilosa kinafanya utafiti wa mahindi, mazao jamii ya mikunde, mtama, uwele, ulezi na alizeti. Anaongeza kuwa, Kituo cha Makutupora kilichopo Dodoma kinafanya utafiti wa zao la zabibu huku kile cha Tengeru Arusha kikitafiti mboga, viungo na matunda. Anasema Kituo cha Selian mkoani Arusha kinatafiti ngano, shayiri na mahindi kwa kushirikiana na kituo cha Ilonga.

Kituo hicho pia kinatafiti maharage kwa kushirikiana na kituo cha Uyole, Mbeya. “Kama nilivyosema, Tari Uyole kinafanya utafiti wa mahindi kwa kushirikiana na Ilonga, lakini pia wanafanya pia utafiti wa maharage, viazi mviringo, pareto pamoja na zana za kilimo,” anasema. Anasema watafiti katika kituo hicho pia wanatengeneza teknolojia mbalimbali zinazolenga kujibu changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima. Mkurugenzi Mkuu huyo wa Tari anawahimiza wananchi kushirikiana na taasisi hizo za kilimo ikiwa ni pamoja na Kituo cha Naliendele Mtwara kinachofanya utafiti wa mbegu za mafuta, hususan karanga na ufuta.

Anasema Naliendele pia wanafanya utafiti wa ubore- shaji zao la korosho. Utafiti wa migomba unafanywa na taasisi ya Maruku iliyopo mkoani Kagera ambayo imekuwa ikipambana katika kutoa elimu kwa wakulima juu ya kukabiliana na ugonjwa wa mnyauko. Kwa upande wa Ukiliguru, Misungwi mkoani Mwanza anasema wanatafiti mazao jamii ya mizizi kama vile mihogo, viazi vitamu na viazi vikuu. Halikadhalika, kituo hicho anasema kinatafiti zao la pamba.

Anasema Kituo chao cha Tumbi kilichopo Tabora kina- tafiti kilimo misitu ambacho mkulima anaweza kupanda machungwa pamoja na miti ama mkulima akapanda mahindi kwenye shamba la miti pamoja na mikorosho na mahindi. Utafiti wa zao la chikichi anasema unafanywa na taasisi ya Kihinga iliyopo mkoani Kigoma ili kuongeza uzalishaji wa michikichi inayotumika katika kuzalisha mafuta ya mawese.

Kuhusu mazao yanayovumilia ukame ambayo kama mtama, uwele na ulezi, Dk Mkamilo anasema yanafanyiwa utafiti ili kuyaboresha zaidi na Kituo cha Tari kili- chopo Hombolo, Dodoma. Aidha, kilimo cha viazi mviringo, mahindi na maharage kinafanyiwa utafiti wa kina katika Kituo cha Kifyulilo kilichopo Mufindi mkoani Iringa. Anasema TAari pia wana kituo kinachotunza vinasaba vya mimea katika mazao mbalimbali (NPGRC) kilichopo mkoani Arusha. “Maana yake ni kwamba, unapofanya utafiti lazima utunze vinasaba ili visije vikapotea,” anasema Mkuru- genzi huyo.

Anasema makao makuu ya Tari yapo Makutupora mkoani Dodoma na ndiyo jicho linaloangalia shughuli zote zinazofanyika katika vituo mbalimbali vya utafiti ambavyo vipo katika ekolojia mbalimbali nchini. Dk Mkamilo anawahimiza wananchi kuwasiliana na watafiti wa mazao mbalimbali katika maeneo yao ili kupata majibu ya changamoto wanazokutana nazo katika kilimo.

“Kaulimbiu ya Tari ni ku- leta mapinduzi ya kilimo nchini,” anasema na kuzidi kusisitiza wananchi kuvitumia ipasavyo vituo hivyo. Mwaka jana Dk Mkamilo aliwataka watumishi wa Tari nchini kote kufanya tafiti zenye tija, zinazolenga kumbadilisha mkulima wa kawaida ili apige hatua zaidi kimaendeleo. Anatoa agizo hilo alipokutana na watumishi wa vituo vyote vya Tari katika mkutano uliofanyika Makutupora, Dodoma baada ya kuvunjwa kwa Idara ya Utafiti na Maendeleo ya Kilimo iliyokuwa Wizarani na shughuli zake kukabidhiwa Tari.

Mkamilo anawakumbusha watafiti na wafanyakazi wote wa Tari kuacha kufanya utafiti wa mazoea usio na tija kwa mkulima na badala yake, wabuni mbinu za kuleta fedha kwenye vituo vyao kwa kuandika miradi mbalimbali. Kutokana na sekta ya kilimo kuchangia asilimia 30 tu ya pato la taifa licha ya sekta hiyo kuajiri takribani asilimia 75 ya Watanzania wote, Dk Mkamilo anasema ni lazima Taasisi hiyo ihakikishe kilimo kinachangia zaidi ya hapo.

Katika mkutano huo, Mkamilo anasema bado mchango wa wataalamu wengi wa kilimo si mkubwa kiasi cha kumbadilisha mkulima na kusaidia maendeleo ya viwanda nchini. Anasema hali hiyo haiwezi kuachiwa ikaendelea. Wiki iliyopita Bunge liliambiwa kwamba Tari imeanza utafiti wa afya ya udongo katika kanda zote saba za ikolojia ya kilimo nchini, hatua itakayowasaidia wakulima kulima kwa tija.

Naibu Waziri wa Kilimo, Omar Mgumba, anasema utafiti huo unalenga kubaini aina ya virutubisho na tabia za udongo katika maeneo mbalimbali nchini ili kutoa elimu kwa matumizi sahihi ya mbolea ya viwandani na ya asili.

Mgumba alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Chambeni, Yussuf Salim Hus- sein (CUF), aliyetaka kujua mikakati ya serikali kuhusu kuendeleza kilimo hai kwa kuwa mbolea za viwandani ni ghali. Anasema utafiti huo umeanza kwa kuchukua sampuli za udongo kutoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kati, Kanda ya Kaskazini na sehemu ya Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro na kwamba, utaendelea katika maeneo mengine na kukamilika Juni 2020.

TANGU maambukizi ya virusi vya corona yabishe hodi nchini Machi ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi