loader
Picha

Mafunzo urasimishaji ‘yalivyoanika’ fursa lukuki Tanga

“MNAJUA kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli inaendelea kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa kuruhusu uwekezaji mkubwa wa kibiashara katika Jiji la Tanga.”

Anasema Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa wakati akifunga mafunzo ya siku sita yaliyolenga kuwajengea uwezo wajasiriamali 1000 wa Jiji la Tanga katika nyanja mbalimbali ili kujua umuhimu wa kufanya biashara kwa kufuata mfumo rasmi yaani urasimishaji biashara.

Katika ufungaji wa mafunzo hayo yaliyofunguliwa Aprili 29, mwaka huu na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Daudi Mayeji na kufungwa na Mkuu huyo wa Wilaya ya Tanga, Mei 7, anasema mafunzo hayo yanayoendeshwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), ni muhimu pia kwa wajasiriamali katika kubaini fursa za kibiashara zinazowazunguka.

Awali, Meneja Urasimishaji Biashara wa Mkurabita, Harvey Kombe alisema mafunzo yanalenga kuwajengea uwezo wafanyabiashara kuhusu fursa mbalimbali za kibiashara kupitia urasimishaji na faida zake katika kukuza uchumi wa taifa.

“Utafiti wa awali umebaini kuwa, zaidi ya asilimia 75 ya wafanyabiashara jijini Tanga, hawajawahi kupata mafunzo rasmi ya biashara, hivyo hawajui kubaini na kutumia fursa mbalimbali za kibiashara zikiwamo za kupitia urasimishaji…,” anasema Kombe. Anaongeza: “Hapa nchini imegundulika kuwa, asilimia 90 ya biashara humilikiwa na mtu mmoja mmoja na nyingi hazina kumbukumbu za biashara.”

Kwa mujibu wa Kombe, wafanyabiashara wengi pia hawajui kutenganisha mali za mmiliki na mali za biashara hali inayoangamiza biashara nyingi. Miongoni mwa mambo muhimu waliyofundishwa wajasiriamali hao, Kombe anasema ni pamoja na maana ya urasimishaji biashara na faida zake, taratibu za kupata leseni ya biashara na faida zake na umuhimu wa kutunza kumbukumbu za biashara na kutenganisha mali binafsi na mali za biashara.

Mengine ni taratibu za kufungua akaunti benki pamoja na kupata mikopo kwa ajili ya kukuza mtaji wa biashara, umuhimu wa biashara kulipa kodi serikalini na namna ya kupanga bidhaa na mbinu bora za masoko. “Wamejifunza pia namna ya kushiriki katika uchumi wa viwanda na umuhimu wa wafanyabashara kuweka akiba katika mifuko ya hifadhi ya jamii. Mambo hayo mkayeweke katika vitendo,” anasema.

Mkuu wa Wilaya anawaam- bia wajasiriamali hao washiriki wa mafunzo akisema: “Mafunzo haya yamewawezesha kujifunza jinsi ya kurasimisha biashara, jambo litakalowawezesha kukuza soko la bidhaa zenu kwani kurasimisha biashara ni jambo linalokupa fursa kama mfanyabiashara, kufanya kazi na taasisi mbalimbali za serikali pamoja na kampuni kubwa kwa mfumo wa zabuni.”

Anaongeza: “Mbali na urasimishaji biashara, mmepata fursa za kujua namna mnavyoweza kuongeza mitaji ya biashara zenu kupitia benki na taasisi mbalimbali za kifedha. Pia, mmetambua umuhimu wa urasimishaji mali hasa ardhi ili ikupatie mtaji.” Katika kuwasisitiza wajasiriamali kuyaweka mafunzo hayo katika vitendo ili yawe na tija kwao, Mkuu wa Wilaya anasema: “Mmejua fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi hasa baada ya kujua ni namna gani mnaweza kuongeza thamani ya bidhaa zenu kupitia Shirika la Maendeleo ya Vi- wanda Vidogo nchini (Sido).”

Anasema serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa kuruhusu uwekezaji mkubwa wa kibiashara katika Jiji la Tanga na kwamba hadi sasa, ipo miradi miwili mikubwa iliyo katika hatua mbalimbali za utekelazaji. Mwilapwa anaitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuzalisha saruji cha Hengya na ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda litakaloishia jijini Tanga.

Anasema: “Uwepo wa kiwanda hiki na bomba hili la usafirishaji mafuta umefungua fursa mbalimbali za uwekezaji katika Jiji la Tanga.” Kwa nyakati tofauti mkuu huyo wa ilaya huyo na Mkuru- genzi wa Jiji la Tanga wanas- ema katika mafunzo hayo kuwa, fursa hizo ni malighafi kwa ajili ya uzalishaji mkubwa wa saruji na kuwapo kwa kampuni kubwa zinazoshughulika na mafuta kuwekeza katika

TANGU maambukizi ya virusi vya corona yabishe hodi nchini Machi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi