loader
Picha

Mkulima wa korosho anayetamani wataalamu kumtembelea

“MIMI ni mkulima wa korosho, nina ekari 200 za mikorosho safi kutokana na mbegu za Naliendele, nimeilea miche hii mpaka imekuwa mikorosho, lakini hakuna mtendaji hapa ambaye amekuja kuniangalia na kuona shida zangu.”

Ndivyo anavyosema Mzee Mohamed Bwela mkazi wa Liwale akisisitiza kuwa, pamoja na ukubwa wa shamba lake, mwaka huu katika msimu ujao wa mavuno anaona huenda hatafanya vyema kwa kuwa hajalipwa fedha zake za korosho.

Anasema pamoja na ukweli kuwa hivi karibuni Rais John Magufuli akiwa ziarani Mtwara alizungumzia kulipwa kwa wakulima, licha ya kuwa na tani zaidi ya 15, maofisa husika hawajawahi kumtembelea ili kuhakikisha shamba lake hali itakayompa fursa ya kulipwa kama wanavyofanyiwa wakulima wengine. Anasema hafurahishwi na kitendo cha baadhi ya viongozi wa wilaya kutotilia maanani daftari la wakulima, ili taarifa ziwe sahihi hasa wanaolima korosho na kuona kwamba wanakagua ukweli kuhusu ukubwa wa mashamba yao.

“Zao hili sasa linakuwa gumu. Naweza kumudu eka 200 kwa kusaidiwa, lakini katika hali hii ya kutolipwa fedha, kwa kuwa nina kilo nyingi za korosho hainipi raha. Walita- kiwa kuja kunikagua ili kusije kuwa na tatizo la kunilipa fedha ili shamba langu niweze kutia vibarua lisiharibike,” anasema Bwela ambaye aliyewahi kuwa bwana shamba katika miaka ya nyuma.

Anasema alipostaafu kazi takriban miaka 20 iliyopita, alimchukua mkewe na watoto wake wakaenda kujifunza kulima korosho katika Chuo cha Naliendele kwa miezi mitatu katika miaka ya 2000. “Mafunzo yale ambayo niliyalipia yalinipatia elimu inayotakiwa mimi na mke wangu na tulipokuja tulifanyia kazi mafunzo hayo na watu wa Naliendele walitufuatilia sana,” anasema.

Anasema watu wa Naliendele hawakufikiria mkulima atataka kupewa mafunzo kwa gharama zake. Na walipoona nia ya dhati walimfundisha yeye, mkewe na watoto kuhusu maana ya kilimo na walipomaliza, walikuwa wataalamu. Kwa mujibu wa mzee huyo, sasa wamefikia hatua kubwa zaidi kwani sasa wanabangua korosho kwa mashine ya mkono. Anasema licha ya kuwapa mafunzo, wataalamu wa Naliendele waliwafuatilia wanafunzi wao na kuwapatia miche bora kutoka kituoni hapo na shamba lake likawa ni la mfano na pia kitalu. Anasema wakati Meck Sadik, akiwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, alifika katika shamba hilo kujifunza na yeye alipewa nafasi ya kushindana kikanda na kitaifa. Katika mashindano hayo ya yaliyofanyika 2015, alikuwa mshindi katika vipengele vingi, lakini anasema taabu anayoipata sasa inatokana na maofisa kilimo kutowatembela wakulima ili kujua changamoto walizo nazo. “Kikubwa zaidi watu wamebaki maofisini zaidi wakiwapatiwa takwimu na wakati mwingine wanapewa takwimu ambazo siyo sahihi na ndiyo maana wengine tunapata shida,” anasema Bwela. Wakati akizungumza pia katika Mkutano wa Chama cha Msingi cha Umoja Amcos cha Liwale akiwa miongoni mwa wanachama, alimtafadhalisha Mkurugenzi wa Hal- mashauri ya Liwale, Luiza Mlelwa kuona haja ya maofisa wa serikali kuwatembelea wakulima na kuwaona na kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili. Mintarafu kuchelewa kwa malipo, anawaomba maofisa na watendaji wanaohusika kuongeza kasi ili wawafikie walengwa wote haraka hali itakayomwezesha yeye na wengine wenye shida kama yake, kuhakikiwa na hivyo, kupata malipo yao mapema. “Nimekuwa hospitali kwa muda mrefu na nimerudi hapa naona dhahiri kwamba kuna shida. Rais amekwisha toa maelekezo kwamba atatulipa, lakini kasi ya baadhi ya viongozi na watendaji inatukatisha tamaa,” anahoji. Anasema katika mahojiano kwamba, wakulima wengi hawana elimu na hawajui elimu hiyo waipate wapi kwani watu wenye dhamana wamebaki ofisini wakifanya kazi wanazodhani ni za wakulima, kumbe za kwao kwa kuwa wakulima wengi hawapati msaada ipasavyo. Kwa mujibu wa mkulima huyo, shida alizo nazo zikiwamo za ukosefu wa fedha, zinamfanya ashindwe kujiandaa na kilimo katika msimu ujao. Anasema: “Kukosekana kwa daftari la wakulima na viongozi wenye hamasa ya kusaidia wakulima kunatufanya wakulima wengi kuwa wapweke kwa kukosa huduma na na hivyo, kukosa utaalamu zaidi na kuchelewa kufanya maandalizi kwa ajili ya msimu mwingine.” Katika mkutano wa Umoja Amcos, wazungumzaji wengi wakiwemo wanachama na bodi walizungumzia haja ya wakulima na hasa wa chama chao kuongeza zao lingine la biashara na kuacha kulitegemea zao la korosho pekee. Uchunguzi wa makala haya umebaini kuwa, kutokana na ununuzi haramu wa korosho uliofanywa na walanguzi kwa kipindi kirefu kupitia mfumo wa kangomba uliowapunja wakulima, serikali mwaka jana iliingilia katika ununuazi wa zao hilo kupitia uhakiki wa mashamba ili kuwabaini walanguzi. Hali hiyo iliufanya utaratibu uliozoeleka wa majukumu ya vyama vya kubadilika kutokana na ukweli kuwa mfumo wa ununuaji wa koro- sho uliwafanya wao wasiwe na nafasi ya kudai fedha walizokubaliana na wakulima ili kuendesha ushirika. Wanachama walikuwa wamejipangia kuiwezesha Amcos hiyo Sh 70 kwa kila kilo ya korosho inayopenya katika mnada, lakini kutokana na mabadiliko ya soko, chama hicho sasa hakiwezi kufanya mambo mengine kwani lengo la kukusanya Sh milioni 300 kama tozo katika mauzo ya korosho limeshin- dikana. Mwenyekiti wa Amcos hiyo, Hassan Mpako katika hotuba kwa wanachama anawasisitiza ukweli kuwa, bado serikali ina nia thabiti ya kulipa wakulima wake wote waliobaki katika korosho na kwamba taratibu lazima zifuatwe ili kila mmpoja apate haki anayostahili. Mpako anawataka wanachama wake kuanza kufikiria kulima mazao mengi mengine na kuacha kasumba ya kutegemea zao moja pekee (korosho). Pamoja na kuwataka wakulima wawajibike, pia anasisitiza haja ya kuendelea kufuata taratibu za malipo na kila mtendaji afanyekazi kwa uadilifu kusaidia wakulima kupata haki zao mapema. Amcos ya Umoja kwa Liwale ilitenga Sh bilioni 9 kama fedha za msimu wa korosho wakitarajia malipo kwa ajili ya mauzo ya korosho, ununuzi wa vifungashio na pia usafirishaji wa korosho na utunzaji katika maghala. Kaimu Mrajis Msaidizi wa Ushirika Mkoa wa Lindi, Robert Msunza anasema wakulima watalipwa korosho zao zote na hata wale wa ‘kangoba’ wametakiwa kuandika barua ya kuomba radhi na mwishoni walipwe. Hata hivyo, Mzee Bwela anakuwa anasema ana shaka kama atafanya kilimo ipasavyo katika msimu ujao wa korosho akisema yeye na baa- dhi ya wakulima wa namna yake, watashindwa kumudu gharama za kupalilia mashamba yao na kuyaweka katika hali ya kupiga dawa na kusubiri mavuno. “Tabia ya mauzo ya korosho, ni ya kutia shaka maana wakati mwingine, kadiri korosho zinanavyo- zidi kukaa, zinakuwa na tatizo la kuharibika na hivyo kukosekana kwa maghala mapya kunaweza kutia doa soko lijallo,” anasema. Hata hivyo anasema, lengo la Rais Magufuli (Serikali) katika zao hilo kwa wakulima ni zuri, isipokuwa kasi ya utendaji ya baadhi ya watendaji, inakuwa changamoto. “Kama huwezi kusaidiwa katika mambo haya, inasikitisha wanapomwambia Rais kwamba kila kitu kipo sawa, wakati kila kitu hakipo sawa na wakulima wenye haki zao kama mimi bado wanataabika,” anasema Bwela.

TANGU maambukizi ya virusi vya corona yabishe hodi nchini Machi ...

foto
Mwandishi: Beda Msimbe

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi