loader
Picha

Magunomics ilivyojielekeza katika miradi ya kimkakati (2)

WIKI iliyopita katika mfululizo wa makala haya yanayojikita katika sera za mageuzi ya kiuchumi zinazotekelezwa na serikali chini ya Rais John Magufuli tunazoziita hapa ‘Magunomics’ tukimaanisha Magu (Magufuli) na nomics (economics yaani uchumi), tuliangalia maeneo muhimu ya kimkakati zinakopelekwa pesa zilizookolewa yakiwamo ya afya, elimu bure, miradi ya maji, ujenzi wa barabara na ujenzi wa reli ya kisasa.

Katika toleo hili, tunaangalia maeneo mengine tukianza na mitambo ya kuzalisha umeme. Serikali ilitekeleza miradi 10 kwenye maeneo mbalimbali nchini ukiwamo upanuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa Gesi Kinyerezi 1 (K1-Extension) na Kinyererzi 2 (K-2). Kinyerezi 1 Extension: Mradi huu wa megawati 185 uliingiza umeme katika gridi ya Taifa Novemba, 2018 huku. Kinyerezi 2: Mradi huu wa megawati 240 ni mtambo wa kwanza wa megawati 30 uliowashwa Desemba, 2017.

Mradi wa usambazaji wa umeme vijijini chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea kwa kasi kubwa. Mpaka sasa zaidi ya wananchi 172,000 kati ya 250,000 wameunganishwa na nishati hiyo. Aidha, serikali imeanza ujenzi wa umeme wa maji ya Bonde la Mto Rufiji (Stiegler’s Gorge). Mradi huo utakapokamilika, utatoa umeme kiasi cha megawati 2,115 huku mahitaji ya Taifa kwa sasa yakiwa megawati 1,560.

Umeme unaotokana na maji ni wa gharama nafuu (Sh 36 kwa uniti) ukilinganishwa na ule wa mafuta (Sh 547 kwa uniti). Kwa maana hiyo, umeme huo utaokoa fedha nyingi. Kufufua shirika la ndege Ili kuongeza mapato ya ndani na fedha za kigeni, Serikali ya Awamu ya Tano iliweka mkakati wa kufufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL). Kwa kutekeleza mkakati huo, serikali iliamua kununua ndege saba kwa pesa zake za ndani na kwa kulipa fedha taslimu.

Hadi kufikia Januari mwaka 2019, ndege sita zilikuwa zimenunuliwa: ndege tatu aina ya Bombardier Q400, ndege moja ya Boeing 787-8 Dreamer na ndege mbili za Airbus 220-300. Ndege hizo zimeanza kwa usafiri wa ndani na kuanzia Februari mwaka 2019 na hata safari za nje. Ni dhahiri kwamba, ununuzi wa ndege hizo utaiongezea serikali mapato zaidi ya ndani na fedha za kigeni kupitia kwa watalii. Aidha, utaharakisha usafiri wa abiria na bidhaa na utaondoa aibu kwa nchi yenye utajiri mkubwa kutokuwa na usafiri wa anga.

Mkakati huo unafanyika pamoja na ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA). Ujenzi huo umekamilika kwa zaidi ya asilimia 80 na ujenzi wa majengo na mahitaji yote utakuwa umekamilika baada ya miezi michache ijayo. Tanzania kuelekea uchumi viwanda Katika juhudi za kujenga uchumi wa viwanda takriban viwanda 3,504 vilianzishwa na kusajiliwa kupitia Brela, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).

Kati ya viwanda hivyo, 2,500 ni viwanda vidogo sana, 943 viwanda vidogo, 51 viwanda vya kati na 10 viwanda vikubwa. Inakadiriwa kwamba, kupitia viwanda hivyo, zaidi ya Watanzania 26,000 wameajiriwa. Ili kuleta usawa, serikali inahamasisha kuanzisha viwanda vinavyotumia malighafi za ndani, vinavyoajiri watu wengi na vitakavyoanzishwa maeneo ya vijijini au kwenye miji midogo. Aidha, kupitia usimamizi na ufuatiliaji wa Msajili wa Hazina, kati ya viwanda 156 vilivyobinafsishwa, mapendekezo yametolewa kuvichukua viwanda 86 ambavyo havijaendelezwa. Ofisi ya Msajili imeshachukua hatua za kurejesha viwanda 14 serikalini ili kuvitafutia wawekezaji wengine walio tayari kuviendeleza.

Mwaka 2017 sekta ya viwanda ilichangia asilimia 5.5. katika Pato la Taifa. Ikilinganishwa na Korea Kusini, uzalishaji wa viwanda ulichangia asilimia 30 kwenye Pato la Taifa mwaka 2016. Kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Shirika la Kimataifa linalojihusisha na Biashara na Maendeleo (UNCTAD) ya mwaka 2017, Tanzania imekuwa ikiongo- za kwa kuvutia wawekezaji kutoka nje miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) kama ifuatavyo: Tanzania –Dola za Marekani Bilioni 1.35, Uganda-Dola milioni 541, Rwanda Dola milioni 410, Kenya Dola milioni 394 na Burundi Dola milioni 0.1.

Maeneo mengine Maeneo mengine ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imefanya na inaende- lea kufanya ni pamoja na upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam; ujenzi wa rada nne za kisasa za kuongezea ndege; upanuzi wa viwanja vya ndege vya kimataifa Julius Nyerere uliopo Dar es Salaam (JNIA), Kilimanjaro (KIA) uliopo mkoani Kilimanjaro. Lingine ni ujenzi wa viwanja vipya vya Songwe na Chato; ujenzi wa meli kubwa yenye uwezo wa kubeba abiria 1200 na tani 400 za mizigo, ujenzi wa cherezo cha kutengeneza meli chenye uwezo wa tani 4000 na ukarabati mkubwa wa meli ya MV Victoria.

Mambo mengine yaliyofanyika ni kuhamisha makao makuu ya nchi kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, mapambano dhidi ya dawa za kulevya na kuanzisha Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, ujenzi wa hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutatua migogoro inayohusiana na ardhi (wakulima na wafu- gaji, wawekezaji na wananchi, serikali na wananchi na wananchi wenyewe kwa wenyewe).

Mengine ni kukomesha mauaji na usafirishaji wa wanyama hai, kuunda kamati ya kuchunguza mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizoibiwa na maandalizi ya ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Tanzania hadi Uganda. Kutekeleza Sera za Kifedha Mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi na utekelezaji wa sera za kibajeti yameondoa mabilioni kama siyo matrilioni ya fedha chafu kwenye mzunguko.

Uwepo wa fedha chafu katika mzunguko, ulisababisha uhaba mkubwa wa fedha na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi. Ili kukabiliana na hali hiyo, serikali ilitekeleza sera za kifedha kwa kuongeza fedha kwenye mzunguko. Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilichukua hatua mbalimbali kuongeza ukwasi kwenye uchumi ili kuziwezesha benki za biashara kuongeza utoaji wa mikopo kwa sekta binafsi. Hatua hizo ni pamoja na kutoa mikopo ya muda mfupi kwa mabenki; kushusha riba ya mikopo kwa mabenki kutoka asilimia 9 hadi asilimia 7 Agosti 2018.

Kutokana na hatua hizo, ukwasi kwenye mabenki ya biashara uliongezeka na riba katika masoko ya fedha zilipungua. Ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi uliongezeka kwa wastani wa asilimia 4.6 (Julai hadi Oktoba 2018) ukilinganisha na wastani wa asilimia 0.2 kwa kipindi kama hicho mwaka 2017.

Sera hizo za upanuzi wa fedha (expansionary policy), ziliwawezesha wafanyabiashara wakubwa na wadogo na wafanyakazi wa serikali na mashirika ya umma kukopa zaidi na kuwekeza kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo.

Matokeo ya Magunomics Kama ilivyoelezwa awali, lengo la “Magunomics” lilikuwa kujenga uchumi imara - uchumi wa viwanda - utakaoiwezesha nchi kufikia Uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025; kupunguza umaskini na kuboresha maisha ya Watanzania na kuiwezesha nchi kujitegemea na kutetea maslahi yake. Matokeo ya utekelezaji wa Magunomics ni makubwa na yajayo yanafurahisha.

TANGU maambukizi ya virusi vya corona yabishe hodi nchini Machi ...

foto
Mwandishi: Profesa Kitojo Wetengere

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi