loader
Picha

IGP Sirro ateua Msemaji mpya Polisi

MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro amefanya mabadiliko ya watendaji ikiwa ni pamoja na kubadili Msemaji wa Jeshi hilo.

Katika mabadiliko hayo IGP Sirro amemteua aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmed Msangi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar.

IGP Sirro amemteua kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) David Misime kuwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Taarifa ya Kamishna wa Ushirikishwaji wa Jamii kwenye jeshi hilo, Mussa Mussa imeeleza kuwa, IGP Sirro amemhamisha aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai Zanzibar Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Maulid Mabakila kumpeleka makao makuu ya Polisi, Dar es Salaam.

DCP Msangi amesema, mabadiliko hayo ni ya kawaida kuboresha utendaji wa Jeshi la Polisi.

SACP Misime amewaomba waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla kuendeleza ushirikiano wa Polisi na waandishi wa habari katika kuielimisha jamii iache vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi