loader
Picha

Wote waliofaulu darasa la 7 waenda sekondari

JUMLA ya wanafunzi 133,747 waliofaulu elimu ya msingi mwaka jana na kukosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa, wameanza masomo, baada ya ujenzi wa vyumba hivyo kukamilika.

Kukamilika kwa ujenzi wa vyumba hivyo, kumetokana na agizo la Rais John Magufuli kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo kuitaka mikoa yote iliyokuwa na uhaba wa vyumba hivyo kuhakikisha wanajenga na kukamilika ifikapo mwishoni mwa Machi, mwaka huu.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, akiwa kwenye ziara ya kutathmini utekelezaji wa agizo la ujenzi wa vyumba hivyo kwenye mikoa iliyokuwa na uhaba, Naibu Katibu Mkuu Tamisemi anayeshughulikia Elimu, Tixon Nzunda alisema wanafunzi wote waliofaulu mwaka jana sasa wamekwenda sekondari.

“Ni rasmi sasa wale wote waliofaulu mwaka jana kujiunga na elimu ya sekondari wamekwenda, baada ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kukamilika, hapa niko kwenye vikao tunafanya tathmini ya utekelezaji wake,” amesema Nzunda.

Mwishoni mwa mwaka jana, Waziri Jafo alitangaza idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na kusema jumla ya waliochaguliwa ilikuwa wanafunzi 599,356 sawa na asilimia 81.76 ya wanafunzi wote 733,103 waliofaulu.

Katika maelezo ya Jafo, wanafunzi 133,747 walifaulu na kukosa nafasi ya kuendelea, hivyo akaagiza mikoa iliyokuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa kuhakikisha wanajenga na wakapewa miezi miwili hadi mwishoni mwa Februari, mwaka huu wawe wamekamilisha ujenzi huo.

Hata hivyo, Nzunda alisema katika kutekeleza agizo hilo, Rais Magufuli alitoa fedha Sh bilioni 29.9 ambazo zilisaidia kujenga vyumba vya madarasa 2,197 katika shule za sekondari hivyo kufanya idadi ya waliofaulu na kukosa nafasi kuchaguliwa tena na kuanza masomo mwaka huu.

“Utaona sasa kwamba wanafunzi wote 733,103 waliofaulu mwaka jana kujiunga na kidato cha kwanza, wamekwenda sekondari, hii ni kwamba asilimia 100 ya waliofaulu wamekwenda sekondari mwaka huu,” alisisitiza Nzunda.

Desemba mwaka jana, Waziri Jafo alisema mikoa tisa pekee ndio ilifanikiwa kuwachukua wanafunzi wake wote waliofaulu kuendelea na kidato cha kwanza huko mikoa mingine 17 ikiwa na uhaba wa vyumba vya madarasa.

Hata hivyo, baada ya agizo hilo mikoa hiyo ilianza kujenga vyumba hivyo na kuongezewa fedha hizo Sh bilioni 29.9 ambazo zimesaidia kujenga vyumba hivyo na kuondoa uhaba uliokuwepo.

Sambamba na hilo, Nzunda alisema ajira zilizotoka hivi karibuni na walimu kupangiwa vituo vya kazi zimesaidia pia kupunguza uhaba wa walimu hususani kwenye masomo ya sayansi na kwamba wizara itaendelea kuboresha mazingira ya elimu kadri inavyowezekana.

Katika hatua nyingine, Nzunda alisema Rais Magufuli ametoa Sh bilioni 35.3 kwa ajili ya kumalizia maboma ya vyumba vya madarasa 2,847 katika shule za msingi kwenye halmashauri 184 Tanzania Bara, yaliyojengwa kwa nguvu ya wananchi.

Alisema ujenzi wa kumalizia maboma hayo ya madarasa utaanza wiki hii na lengo ni kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani.

Nzunda alisema fedha hizo tayari zimeshatumwa kwenye akaunti za shule husika na kwamba wana imani kuwa ujenzi ukikamilika, shule nginyi za msingi zitapunguza msongamano wa wanafunzi kwenye darasa moja na pia utasaidia kuondoa uhaba wa vyumba

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi