loader
Picha

Aussems ahamishia hasira kwa Mtibwa

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema baada ya kushindwa kupata matokeo mazuri katika mechi mbili zilizopita, vita yao inahamia kwa Mtibwa Sugar na Ndanda wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri.

Katika mchezo wa juzi uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, wekundu hao wa Msimbazi walilazimishwa suluhu dhidi ya Azam FC. Kabla ya mche- zo huo, walitoka kufungwa bao 1-0 na Kagera Sugar na kupoteza pointi nne tofauti na matarajio yao. Akizungumza baada ya mchezo huo dhidi ya Azam FC , Aussems alisema wanahitaji pointi sita katika mechi zijazo hivyo mawazo yao yote wanahamishia huko.

“Tuna mechi Alhamisi (kesho) na Jumapili dhidi ya Mtibwa na Ndanda ambazo ni muhimu kwetu kuhakikisha tunashinda ili kuwa katika mazingira mazuri ya ushindi, nina imani tutafanya vizuri,” alisema. Kocha huyo alitaja kilichosababisha wao kushindwa kupata ushindi katika mechi yao ya juzi kuwa ilitokana na wapinzani wao kucheza kwa kujilinda.

Alisema walijaribu kila njia kupata matokeo kwa kucheza mipira mirefu, kona, waliten- geneza nafasi nyingi na kutawala mpira kila upande lakini haikusaidia kutokana na aina uchezaji wa Azam FC. Aussems alisema katika mchezo kama ukishindwa kupata pointi tatu basi angalau kupata pointi moja na ndicho walichopata na wanashukuru na kusahau wakielekeza nguvu zao katika michezo inayokuja. Kwa upande wake Kocha wa Azam, Idd Cheche alisema hawakutaka kurudia makosa ya mchezo wa raundi ya kwanza kwa kupoteza tena hivyo, alitizama mbinu za Simba na kutumia kujipanga.

Alisema lengo lao ilikuwa ni kushinda lakini walipata sare huku akitolea sababu kuwa uwanja ulikuwa na maji na kushindwa kucheza soka la burudani na kwamba kama wangecheza uwanja mkavu basi mambo yangekuwa mazuri. “Katika mchezo wa raundi ya kwanza sikuwepo katika benchi lakini nilitizama ule mchezo ili tusije kurudia makosa tukajipanga na zaidi tulitaka pointi tatu ila tumepata sare tunashukuru na kujipanga kwa michezo ijayo,” alisema.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi