loader
Picha

Wilaya 3 Dodoma kukosa umeme

WILAYA tatu za mkoani Dodoma ikiwa ni pamoja na baadhi ya maeneo ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma leo zitakosa huduma ya nishati ya umeme.

Taarifa iliyotolewa jijini jana hapa na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu, kukosekana kwa nishati ya umeme kunatokana na kufanyika matengenezo makubwa ya kubadilisha nguzo chakavu katika laini ya Msongo Kv 33.

Alisema umeme huo utakosekana siku ya leo kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa 11 jioni. Taarifa hiyo ilisema:

“Shirika linawaomba radhi wananchi kwa usumbufu utakaojitokeza katika maeneo amabayo yataathirika na tatizo hilo”.

Katika taarifa hiyo, Temu alitaja maeneo ambayo yataadhirika na tatizo hilo kuwa ni baadhi ya maeneo ya Ihumwa na Nane Nane, Hombolo yote na Nzuguni yote kwa upande wa maeneo ya Jiji la Dodoma.

Alisema pia umeme utakosekana katika wilaya za Mpwapwa, Kongwa na sehemu ya maeneo ya Wilaya Chamwino na Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.

Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri alibainisha kuwapo tatizo la kukatikatika umeme katika wilaya yake.

Alisema njia pekee ya kuondokana na tatizo hilo ni kutekelezwa kwa mradi wa kuweka vituo vipya vya umeme katika kila baada ya kilomita 80, jambo ambalo litasaidia upatikanaji wa uhakika wa nishati hiyo.

Pia Shekimwei alitumia fursa hiyo kupongeza Wakala wa Umeme Vijijini (REA) na Tanesco kwa juhudi za kufikisha umeme katika vijiji vya Wilaya ya Mpwapwa na kuongeza kuwa huduma ya umeme itasaidia kuboresha huduma za kijamii na maendeleo ya uchumi.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi