loader
Picha

Man City hatihati kufungiwa Ulaya

WACHUNGUZI wa Uefa wanataka Manchester City ifungiwe kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa kama watabainika kuvunja sheria za matumizi ya fedha.

Aidha, kwa mujibu wa vyanzo vya habari, maamuzi ya mwisho hayajafanywa bado na kiongozi wa uchunguzi huo Yves Leterme. Waziri mkuu huyo wa zamani wa Ubel- giji, ambaye ndio mwenyekiti wa kamati hiyo ya uchunguzi ambayo ni kamati huru ya Uefa, anatarajiwa kutoa maoni yake wiki hii.

Pamoja na hayo lakini wajumbe wake wametoa maoni kwamba City inastajili adhabu ya kufungiwa kwa msimu mzima kama itabainika imefanya makosa kwenye matumizi ya fedha. Leterme na watu wake wamekuwa akitafuta vielelezo katika taraifa zilizotolewa na gazeti la Ujerumani Der Spiegel mwaka jana.

Taarifa hizo zilisema kuwa Manches- ter City imevunja kanuni za matumizi ya fedha kulingana na thamani yao ya ufadhili. City iliwahi kupigwa faini ya pauni milioni 49 mwaka 2014 kwa makosa ya kuvunja kanuni.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu wamekanusha tuhuma hizo na Uefa imesema haitazungumza chochote kutokana na uchunguzi huu unaoendelea lakini kwa mujibu wa New York Times, wachunguzi hao wanataka City iadhibiwe kwa kifungo. Uefa inaweza kukubaliana na maoni ya Leterme yanayotarajiwa kutoka baada ya siku mbili na inaonekana haitafanya kazi kwa msimu ujao kwasababu City inaweza kukata rufaa na inaweza pia kufika mpaka mahakama ya michezo ‘CAS’.

foto
Mwandishi: MANCHESTER, England

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi