loader
Picha

Ma-RC waagizwa kuhimiza viwanda mifuko rafiki

WAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kutumia fursa ya tamko la serikali la kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya mifuko rafiki wa mazingira.

Pia, wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kutekeleza ajenda ya serikali ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki katika maeneo yao.

Agizo hilo lilitolewa jana jijini hapa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo.

Alisema ni vyema wakuu wa mikoa wakahamasisha ujenzi wa viwanda vya mifuko mbadala ambavyo vitasaidia upatikanaji wa bidhaa hiyo na kutoa ajira katika maeneo yao.

“Mifuko ya plastiki haitatumika tena, pia kuna fursa ya ujenzi wa viwanda, jambo hili litupe nafasi ya kuangalia jinsi gani katika kampeni yetu ya ujenzi wa viwanda vidogo tunaweza kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya mifuko mbadala vya kati na vikubwa, tutumie fursa hii,” alisema.

Aliongeza: “Mnakumbuka katika kampeni yetu ya miezi 12 ya kila mkoa kujenga viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vipatavyo 100, lengo letu ilikuwa vijengwe viwanda 2,600 lakini tukajikuta viwanda 4,887 vimejengwa.”

Alisema kiwango hicho ni kikubwa hivyo bado fursa ipo ya wakuu hao wa mikoa kutumia katazo la serikali kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya mifuko rafiki wa mazingira kwani mlango mmoja ukifungwa fursa maeneo mengi ya viwanda hufunguliwa.

Aidha, Jafo aliwataka kuhakikisha wanasimamia ipasavyo katazo la mifuko ya plastiki katika maeneo yao ili kuiwezesha Tanzania kuungana na nchi zilizokataa kutumia bidhaa hiyo.

“Juni Mosi, mwaka huu, itakuwa mwanzo wa kutotumia mifuko ya plastiki, wakuu wa mikoa mna dhamana, tukiamua kukomesha hili kwa kuhakikisha mnaunga mkono ajenda ya serikali ya kupiga matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo imekuwa na madhara ya kiafya na kimazingira,” alisema.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi