loader
Picha

Tulipanga kuoana na Ruge -Nandy

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Faustina Mfi nanga ‘Nandy’ ameweka wazi kuwa ni kweli alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa mkurugenzi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba aliyefariki dunia Februari mwaka huu.

Kwa nyakati tofauti, kabla ya Ruge kufikwa na umauti, Nandy alikanusha taarifa za kuwa naye kwenye uhusiano wa kimapenzi, akidai hawezi kutoka naye kwani alimchukulia kama baba yake.

Kwa mujibu wa mahojiano na Millard Ayo tv, Nandy alisema hawakutaka kuweka hadharani uhusiano wao kwa kuhofia uzushi na maneno yasiyofaa kutoka kwenye mitandao ya kijamii na kuongeza kuwa walikuwa na mipango ikiwemo kufunga ndoa. “Hatukupenda mahusiano yetu yaendeshwe na mitandao ya kijamii, najua ingekuwa wazi ingekuwa mbaya zaidi, kuna watu wangeona ni sawa na wengine sio sawa,”alisema Nandy.

“Tulipanga kufunga ndoa ndio Machi (mwaka) huu… nammiss kwa sababu sikuwa nafanya kitu bila kumshirikisha,” alisema. Aliongeza kuwa walikuwa wametambulishana katika familia zao na kwamba ndoa yao isingekuwa ya siri kama yalivyokuwa mahusiano yao. Kuhusu kuugua kwa Ruge, Nandy alisema Ruge hakuwahi kukata tamaa kwa wakati wote waliokuwa akiugua.

“Hata wakati anapeleka Afrika Kusini si kwamba alikuwa amekata tamaa kimaisha ila alipelekwa mbali kidogo ili aelekeze mawazo yake kwenye matibabu maana akiwa hapa (Tanzania) alikuwa akiwaza kazi.” Nandy alisema, anashindwa kumsahau Ruge na mpaka sasa bado ana jumbe zake walizokuwa wanatumiana kwenye simu na anashindwa kuzifuta. “Kuna vitu alikuwa ananiambia nikipitia meseji nashindwa hata kufuta, yaani naishi kwenye zile meseji.”

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi