loader
Picha

Mtoto wa R. Kelly afukuzwa chuoni

ACHANA na rundo la kesi zinazomuandama R. Kelly mahakamani na tetesi za kufi lisika kwake, ripoti mpya zinasema kwamba mtoto wake, Joann Lee amezuiliwa kuingia darasani na kurudishwa nyumbani kutokana na kutokamilisha karo.

Imeelezwa kwamba juzi Lee alifika chuoni lakini hakuingia darasani kutokana na madai hayo ambapo meneja wa Kelly, Darrell Johnson amejaribu kuweka mambo sawa kwamba si kweli Kelly ameshindwa kulipa fedha hizo isipokuwa alisitisha kufanya hivyo baada ya kusikia Lee ameacha chuo tangu mwaka 2018.

Imefafanuliwa kwamba Kelly yupo tayari kulipa ada hiyo lakini mpaka atakapooneshwa mtiririko wa malipo hayo kama kweli fedha hizo zinafika chuo kwa kupewa stakabadhi husika za malipo yake. Taarifa zinaeleza kuwa Lee hana mahusiano mazuri na nguli huyo wa muziki duniani kutokana na shutuma za unyanyasaji wa kingono zinazomuelemea kwa sasa hivyo kusababisha kukosekana kwa mawasiliano mazuri juu ya maendeleo ya elimu yake.

UONGOZI wa klabu ya Chelsea umempa ruhusa kiungo wake N’golo ...

foto
Mwandishi: CALIFORNIA, Marekani

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi