loader
Picha

Dar kuelimishwa athari mifuko ya plastiki

HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam itaanza kutoa elimu kwa jamii kuhusu athari za mifuko ya plastiki kwa kutumia mfumo wa matangazo ya umma katika Manispaa zake zote kuanzia Ijumaa.

Mkuu wa Idara ya Udhibiti Taka na Hifadhi ya Mazingira wa Jiji la Dar es Salaa, Shedrack Maximilian alieleza hayo alipozungumza na gazeti hili kuhusu zuio la serikali la matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia Juni Mosi, mwaka huu.

Alisema Jiji la Dar es Salaam linalokadiriwa kuwa na watu milioni sita lina shughuli nyingi, zikiwemo za viwanda na biashara hivyo limeathirika kwa kiasi kikubwa na mifuko ya plastiki.

“Kuanzia Ijumaa Jiji litaanza kutoa elimu kwa kutumia magari. Yatatolewa matangazo kwenye maeneo yote ya Jiji lakini vile vile kutakuwa na kikao wiki ijayo cha wataalamu wa mazingira wa Manispaa ili na wao waweke mipango ya namna ya kutoa elimu ya madhara ya mifuko ya plastiki,“ alisema Maximilian.

Alisema wananchi wa Jiji la Dar es Salaam wanapaswa kuwa wa kwanza kupinga matumizi ya mifuko ya plastiki kwa sababu inaleta athari nyingi, zikiwemo kuziba mifumo ya majitaka hivyo kusababisha mafuriko na pia kuathiri viumbe hai wa baharini.

“Mifuko ikiishaingia kwenye bahari inaharibu idadi ya samaki. Kama dunia haitazuia mifuko ya plastiki itafikia hatua mifuko ya plastiki kwenye vyanzo vya maji na mazalia ya samaki itakuwa ni mingi kuliko hata samaki wenyewe.

“Wananchi waanze sasa kuzoea kutumia mifuko mbadala. Miaka ya tisini hii mifuko ya plastiki haikuwepo, ilikuwa ikitumika hiyohiyo mifuko mbadala na vifaa mbadala,” alisisitiza Maximilian.

Alisema mifuko mbadala ya kubeba bidhaa kama vile magunia, ndoo na sufuri bado ipo na kwamba kinachotakiwa ni mabadiliko ndani ya jamii.

Hivi karibuni Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, ilipiga marufuku uzalishaji, uuzaji, usafirishaji nje ya nchi, usambazaji, uuzaji na matumizi ya mifuko ya plastiki ifikapo Juni Mosi, mwaka huu.

Kwa mujibu wa katazo hilo adhabu za faini au vifungo zitahusika kwa atakayekiuka katazo kulingana na kanuni za marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki za mwaka 2019 zilizoandaliwa chini ya Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004.

Faini zitakazotozwa ni pamoja na Sh milioni 20 kwa kuingiza nchini mifuko ya plastiki, Sh milioni 20 kwa kusafirisha nje ya nchi, Sh milioni 10 kwa kuzalisha, kuhifadhi na kusambaza, Sh 10,000 kwa kuuza na Sh 30, 000 kwa kutumia mifuko ya plastiki.

Katazo hilo pia linasema bidhaa ambazo hazitaathiriwa na katazo hilo ni pamoja na vifungashio vya dawa, vyakula kama vile maziwa, korosho, bidhaa za viwandani,

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Jeremiah Sisya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi