loader
Picha

Upelelezi kesi bosi NIDA haujakamilika

UPELELEZI katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu na wenzake, haujakamilika.

Wakili wa Serikali, Janeth Magoho alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa. Magoho aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama upelelezi umekamilika au la.

Hakimu Mmbando aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 28, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Maimu na wenzake wanakabiliwa na mashitaka ya kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 1.175.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Biashara wa NIDA, Aveln Momburi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 100 kati ya hayo, 24 yakiwa ni ya utakatishaji fedha zaidi ya Sh bilioni 1.1, 23 ya kughushi nyaraka; 43 ni kuwasilisha nyaraka za uongo ili kumdanganya mwajiri wao na kuisababishia mamlaka hiyo hasara.

Mashitaka mengine ni ya kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu (mawili), shitaka moja la matumizi mabaya ya madaraka na mashitaka mawili ya kula njama.

Wanadaiwa kati ya Julai 19, mwaka 2011 na Agosti 31, mwaka 2015, washitakiwa wakiwa maeneo tofauti tofauti ndani ya Jiji la Dar es Salaam walikula njama ya kufanya udanganyifu wa Sh bilioni 1.175 dhidi ya NIDA.

Maimu na Raymond wanadaiwa Novemba 7, mwaka 2011 wakiwa Makao Makuu ya NIDA, Kinondoni, walitumia madaraka yao vibaya na kusababisha Kampuni ya Gotham International Ltd na kupata faida ya Sh 899,935,494.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi