loader
Picha

Wakenya kortini kwa kufundisha bila kibali

WALIMU wanne ambao ni raia wa Kenya, wanaofundisha Shule ya Msingi na Sekondari ya Kings na Mtanzania mmoja, wamefi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali.

Washitakiwa hao ni Esrom Maina, (45), Ruth Njuguna (30), Joseph Kuria (30), Charles Sakawa (32) na mtanzania Stella Bizulu (44). Akisoma mashitaka hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile, Wakili wa Serikali, Faraji Nguka, alidai washitakiwa walitenda makosa hayo kati ya Septemba mwaka 2018 na Machi 18, mwaka huu katika shule ya Msingi na Sekondari ya Kings iliyoko eneo la Goba ndani ya Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Nguka alidai washitakiwa hao raia wa Kenya walikutwa wakifanya kazi ya ualimu katika shule hiyo bila ya kuwa na kibali kutoka Idara ya Uhamiaji. Katika mashitaka ya pili inadaiwa siku na mahali hapo mshitakiwa Bizulu, akiwa kama Meneja wa shule hiyo, aliwaajiri walimu hao bila ya kuwa na kibali cha kufanya kazi nchini kutoka Idara ya Uhamiaji. Hata hivyo, washitakiwa hao wamekana kutenda makosa hayo na wameachiwa kwa dhamana hadi kesho ambapo upande wa mashitaka unatarajiwa kufanyia mabadiliko hati ya mashitaka.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi