loader
Picha

Ubakaji washika kasi

Tangu Sheria ya Makosa ya Kujamiana (SOSPA) ipitishwe 1998, ubakaji umeendelea kuongezeka, Bunge limetaariwa leo Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile ameeleza leo Jumatano Bungeni, jijini Dodoma kuwa, mnamo mwaka 2015, matukio 394 ya ubakaji yaliripotiwa.

Kuthibitisha kuwa makosa hayo yanaongezeka, Dk Ndugulile alisema hadi kufikia Desemba, 2017, idadi ya waathiriwa ma vitendo hivyo vya kikatili iliongezeka na kufikia 2,984.

Naibu Waziri amelazimika kutoa takwimu hizo baada ya Mbunge Viti Maalum, Najma Giga kutaka kujua idadi ya walioathirika katika matukio hayo tangu SOSPA ipitishwe bungeni.

fHata hivyo, Naibu huyo alisema kuwa serikali inachukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa matukio hayo yanapungua. “Serikali inafanya kazi na vikundi mbalimbali na kuandaa namba maalumu ya kuripoti matukio hayo ambayo ni 116,” ameongeza.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi