loader
Picha

Kanisa Katoliki Dar laja na bima ya 'mkono wa pole' kwa wafiwa

Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Acclavia (Acclavia Insurance Broker) imeanzishwa Bima ya Maisha itakayokua ikitoa mkono wa pole kwa wafiwa pale mwanafamilia anapoaga dunia.

Akizungumza wakati wa mafunzo kwa baadhi ya vikundi mbalimbali vya Kanisa kwa nia ya kuisambaza elimu ya Bima hiyo kwa jamii, mratibu wa mradi wa Bima ya Afya na Maisha wa Acclavia, Agnesi Magimba amesema:

"Tumekuwa tukishuhudia familia zikihangaishwa na shughuli za misiba kwa kuchangisha ndugu jamaa na marafiki. Kwa hiyo tumeamua kuja na huduma hii ili kurahisisha huduma katika kipindi chote cha msiba."

Kima cha chini cha familia ni Sh 18,000-/ kwa mwaka, kwa huduma ya wanafamilia nane pale wanapoaga dunia. Huduma ya msiba ni  kiasi cha Sh 1.5 milioni kwa kila kifo.

“Familia itakayochangia 30,000 kwa mwaka itapewa huduma ya kiasi cha Sh milioni 3, kwa idadi ile ile ya wanafamilia nane wakiaga dunia,” amesema Mratibu.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Abela Msikula

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi