loader
Picha

Bilionea- Fanyeni tendo la ndoa siku 6 kwa wiki

TAJIRI namba moja nchini China ambaye pia ni mwanzilishi mwenza na mmiliki wa kampuni ya kimataifa ya Ali Baba, Jack Ma (54), amewaeleza wafanyakazi wake kuwa, wanapaswa kufanya tendo la ndoa mara sita katika siku sita za wiki na pia wazingatie muda watakaotumia kufanya tendo hilo.

Bilionea Ma amewaeleza wafanyakazi hao kuwa, wapaswa kukutana kimwili wakizingatia kanuni ya 669 ikiwa na maana ya kufanya tendo la ndoa mara sita, siku sita za wiki na kuzingatia muda wa kufanya tendo hilo.

Ameyasema hayo kwenye makao makuu ya kampuni hiyo, Hangzhou wakati wa harusi ya pamoja ya wafanyakazi wa kampuni ya Ali Baba huku akisisitiza kwamba, kanuni ya ‘669’ itawasaidia kuboresha utendaji wao kazini.

Hivi karibuni, Ma alitoa kanuni nyingine iitwayo ‘996’ inayowataka wafanyakazi wa Ali Baba wafanye kazi kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa tatu usiku kwa siku sita za wiki. Ma amesema, kanuni ya 996 ni baraka kubwa kwa wafanyakazi vijana.

“Kazini tunasisitiza ari ya ‘996’, kwenye maisha tuzingatie 669, 669 ni nini? Siku sita, mara sita, na muhimu zaidi ni muda wa kufanya tendo hilo” amesema Ma. Bilionea huyo pia ametoa mwito kwa wanandoa hao wapya wapate watoto.

“KPI ya kwanza ya ndoa (kipimo cha ufanisi kwenye ndoa) ni matokeo, lazima kuwe na mazao, mazao ni nini? Pata watoto” amesema Ma.

Ma ni mwalimu wa zamani wa somo la kingereza, na 1999 alishirikiana na wenzake kuanzisha kampuni ya mtandaoni ya Ali Baba iliyomuwezesha kuwa mtu tajiri zaidi nchini China.

KILA mmoja ana njia yake ya kuonesha heshima ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi